Log in
MWANAKWEREKWE ENVIRONMENTAL ETHICS AND CULTURAL ORGANIZATION (MEECO)

MWANAKWEREKWE ENVIRONMENTAL ETHICS AND CULTURAL ORGANIZATION (MEECO)

Zanzibar, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Katibu wa MEECO Ndugu Suleiman Jeni Pandu akimkabidhi andiko la Mradi "Uwezeshwaji kwa maendeleo" Mh. Haroun Ali Suleiman, waziri wa kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua andiko hilo. Makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwake Mwanakwerekwe

Katibu wa Jumuiya ya MEECO ndugu Suleiman Jeni Pandu akimkabidhi Taarifa ya Mafanikio na Changamoto za wanajamii wa wilaya ya Kusini,  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mh. Ali Mohammed Shein katika kijiji cha jozani alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Mikoa yote ya Zanzibar kuangalia Miradi mbalimbali ya Meendeleo Mikoani humo.

Wanachama na viongozi wa MEECO walioshiriki katika mafunzo ya utawala bora ndani ya Asasi. Mafunzo hayo yalidhaminiwa na shirika la the foundation for Civil Society la Dar-es-Salaam. Kuanzia upande wa kulia walioinama ni katibu wa Asasi ambae pia ni Mratibu wa Mradi huo Ndugu Suleiman Jeni Pandu, akifatiwa na Mwenyekiti wa Asasi Ndugu Abdallah Ali Hassan

Kwa upande wa Asasi yetu ya MEECO nasisi tunatoa salamu za rambirambi kwa familia za ndugu zetu waliopoteza maisha yao katika mafuriko yaliyotokea. Tunapenda kuungana nao kwa hali na mali kwa upande wa shirika letu la envaya tunashukuru sana kwa kuwa karibu na jamii kila linapotokea janga.

large.jpg

Vijana hatarishi katika masuala ya uharibifu wa mazingira kwa kuchimba mchanga walio jaa katika Mji wa Mwanakwerekwe, vijana hawa vilevile hutumia bangi na madawa ya kulevya ili kujipatia vipato vyao na huwa hatari sana kwa wapenda maendeleo kwani huwa wanachukuwa silaha mbalimbali katika harakati zao za haramu

large.jpg

Baadhi ya vitendea kazi katika usafi wa mazira alivyovitoa MH.HAROUN ALI SULEIMAN moja ya ahadi alizoahidi katika uzinduzi huo

large.jpg

MH.HAROUN ALI SULEIMAN Waziri wa kazi na Uwezeshaji Wanaachi Kiuchumi na Ushirika akilopokuwa akifunguwa jumuiya ya MEECO

large.jpg

Viongozi na wanachama wa jumuiya ya MEECO wakiwa katika ziara yao ya kuhamasisha jamii kuhusu utunzaji na uhifadhi wa mazingira ya mikoko katika kijiji cha Unguja Ukuu Mkoa wa Kusini Unguja

large.jpg

Katibu wa MEECO (shati la machungwa) akiwa mgeni rasmi katika Mkutano mkuu wa Jumuiya Rafiki ya UWEMAJO ya Jozani Mkoa wa Kusini Unguja. Suala la utunzaji wa mazingira kuhusu kuepuka ukataji ovyo wa miti ndio mada kubwa aliyoizungumzia.Kushotoni kwake ni Katibu Mtendaji wa jumuiya ya UWEMAJO Bw. Hassan Khatibu akifuatiwa na Msaidizi Katibu wa jumuiya hiyo Bw. Rajab Mchumi ( Mzee Liliondo)

large.jpg

Viongozi na wanachama wa jumuiya ya MEECO wakiwa katika ziara yao ya kuhamasisha jamii kuhusu utunzaji na uhifadhi wa mazingira ya mikoko katika kijiji cha Unguja Ukuu Mkoa wa Kusini Unguja. Kuanzia kulia ni Abdallah Saleh Fatawi (Naibu Katibu)Hija Ramadhan Choko ( Mkuu wa Kamati ya Mapambo)