Injira
Lindi Region Association of Non Governmental Organizations

Lindi Region Association of Non Governmental Organizations

Manispaa Lindi, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Lindi Region Association of Non Governmental Organizations (LANGO) ni Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkoa wa Lindi. Mtandao ulianzishwa rasmi tarehe 20 Juni,2007 na wanachama 5 waanzilishi ambao ni Mitandao ya Asasi Za Kiraia ya Kiwilaya za Mkoa wa Lindi ambayo ni pamoja na; LINGONET (Lindi), KINGONET (Kilwa), ULIDINGO (Liwale), NANGONET (Nachingwea) na RUANGONET (Ruangwa). LANGO imesajiliwa rasmi Septemba 2008 chini ya Sheria Na. 24 ya NGOs ya mwaka 2002 kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto (WMJJW) na kupatiwa cheti nambari 08NGO/00002518. Hadi sasa LANGO imeweza kupata mafanikio mengi yakiwamo haya yafuatayo:-

1. Kufahamika ndani na nje ya Mkoa wa Lindi.

2. Kushiriki katika matamasha na mikutano mbalimbali ya kitaifa.

3. Kuendesha midahalo ya Ulingo wa Maendeleo katika Mkoa wa Lindi.

4. Kushiriki katika Vikao vya Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Lindi (RCC).

5. Kushiriki kikamilifu katika michakato ya mapitio ya MKUKUTA I na ukusanyaji maoni ya wadau wa Mkoa wa Lindi kuhusu rasimu ya MKUKUTA II. 

6. Kuahirikiana na idara, taasisi na Serikali katika ngazi tofauti kwenye Mkoa wa Lindi.

7. Kukubalika na jamii na wadau mbalimbali wa maendeleo.