Envaya

Watoto wakihamasisha wenzao wenzo kwa maandamano ndani ta mtaa wa matopeni, katika maandamano hayo watoto walionesha michezo ya kupuliza bubles zitokanazo na povu la sabuni yenye rangi.Michezo ya watoto ikiandaliwa mahali maalum, huleta maana na huwakutanisha na kujenga uwezo wa kuvumiliana. hapo juu ni maandalizi ya kutengeneza povu la sabuni iliyochanganywa na rangi kwa ajili kupuliza na kurusha bables angani. Mchezo huu ni sawa na ule tuliocheza zamani tukienda kufua nguo mtoni,unafikicha sabuni na kisha kupuliza katikati ya viganja na bables kuruka angani.Katika kudumisha mira na desturi, ngoma za asili zina nafasi kubwa ya kutunza kumbukumbu ndani ya ubongo wa mtoto. Hapa watoto wadogo wanacheza ngoma za asili.Ubunifu hutokana na kutenda, hivyo ni vipande vya nyumba vilivyosambaratishwa na vikiungashwa kwa ustadi unapata nyumba kamili. Watoto wakipewa kazi kama hii huongeza concetration power na uvumilivu katika kila jambo. Katika mradi wa nyumba ya michezo ya watoto, kuna kuunganisha viande vya picha mbalimbali kwa kufuata maelekezo ya picha. Katibu mkuu wa shirika hapo juu naye akijaribu kuunganisha vipande vya tembo kwa kufuata maelekezo ya picha.Hapo juu ni reli iliyounganishwa na treni ikitembea.

 

Kuweza kufanya kazi kwa maelekezo ya mchoro ni mbinu muhimu sana itakayowezesha kuwa makini karibu katika kila kazi.

Mzazi ni muhimu sana kufuatilia harakati za ujifunzaji wa mtoto,huweza kumjengea imani mtoto na kuongeza uwezo wa kujiamini.

 

 

Watoto kufanya kazi za ubunifu kwa pamoja hujenga hulka ya ushirikiano na kuthamini uwezo wa kila mshiriki.

 

Ujifunzaji kwa vitendo ni muhimu ili kupanua uwezo wa kupambana na changamoto za kila siku zinazojitokeza katika jamii.

 

 

Watoto na michezo hawawezi kutenganishwa,inafurahisha na kuongeza hamasa  katika makuzi ya ubongo wa mtoto, na mtoto anapocheza na mzazi/mlezi humfanya kuona umuhimu wa kushirikiana katika nyanja mbalimbali, humpa mtoto pia nafasi ya kueleza hisia zake na ndipo mzazi anaweza kutambua karama zake na hivyo kumuonesha njia ya kufikia kule mtoto anakopenda.