Community Empowerment Development Organization yaani Shirika la kuendeleza ustawi wa jamii kiuchumi na kijamii, ambalo linajishughulisha na maswala ya kuendeleza Kilimo, Mifugo na ustawi wa jamii katika nyanja mbalimbali - zikiwemo huduma za maji, afya, elimu na huduma za uzalishaji/ kuongeza kipato katika kupambana na umaskini miongoni mwao.ni shirika lisilo la serikali lenye namba ya usajili 00NGO/00003075 ya tarehe 22 Aprili 2009.Eneo la shughuli ni Tanzania bara.Tangu kuanzishwa kwake limefanikiwa katika kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wanawake,kusaidia watoto yatima,kufundisha mawakala wa pembejeo za kilimo n.k