DIRA {VISION}YA WATU
Kuwa na jamii ambayo inatambua uwezo na nafasi ya mwanamke katika kuleta maendeleo na fikra potofu kuwa mwanamke hawezi kuzifanya
DHIMA{MISSION}YA WATU
Kutambua fursa na jitihada mbalimbali juu ya jitihada za maendeleo zinazofanywa na wanawake na kuziweka wazi,Pia wanawake wanatumia ujuzi,Maarifa na vipaji vyao kadri wawezavyo na hivyo kuwa shahidi wa uwezo wao katika kufanya shuguli za maendeleo.
MADHUMUNI YA WATU
[1]. Kujenga wanawake,Watoto,Wazee,Vijana katika uwezo wa kiuchumi,Kielimu na uongozi.
[2]. Kusaidia kuboresha afya za wanawake wajawazito,Watoto na jamii kwa ujumla na kuwapa
elimu kuhusu lishe,Kujikinga na maradhi
[3]. Kuboresha hali ya lishe,Uzalishaji na usindikaji wa chakula kwa kusaidia na tiba katika
kilimo na ufugaji.
[4]. Kuboresha mazingira na usafi wanapoishi na maeneo ya kufanyia kazi
[5]. Kukuza vipaji vya watoto wa kike wanawake na vijana kwa ujumla kwa kufuatilia semina na mafunzo mbalimbali kutambua vipaji vyao na masoko.
[6]. Kuhamasisha uendelezaji wa michezo mbalimbali sanaa na utamaduni mashuleni,vyuoni, na vijijini.
[7]. Kupinga na kukemea aina zote za unyanyasaji wa kijinsia,uonevu,na uvunjaji wa haki za binadamu kufanya jamii itambue haki zao na kuwapeleka kunakohusika.
[8]. Kusaidia kujenga hali ya amani,upendo na ushirikiano kwa kutumia wataalamu mbalimbali
katika kutoa elimu kwa jamii.
Viongozi wa Wanawake Tunaweza {WATU} wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Jordani Rugimbana Tarehe 07/09/2012. Siku hiyo ya Semina
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh.Jordan Rugimbana aliyezindua semina ya mchakato wa uundajiwa katiba mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Akizungumza na wanasemina iliyoandaliwa na Asasi ya Wanawake Tunaweza. {WATU} Tarehe 07/09/2012.Kunduchi Tegeta Mtaa wa Pwani.
Mk.JORDuu wa wilaya ya Kinondoni[Mh.Jordan Rugimbana] akiwa katikati ya viongozi wa WATU wakati wa semina
mwenyekiti wa WATU akifafanua kitu katika semina ya mchakato wa uundaji wa Katiba mpya