Log in

/BWJMT/projects: English: WIoe9kuQJPd952HtWHatZnjw:content

« Previous   ·   Next »
Base (English) English

Baraza la Watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunafanya kazi zifuatazo:

 

Kutayarisha mikakati ya kukuza ushirikishwaji wa watoto kwenye mambo yanayowahusu watoto katika ngazi zote kuanzia kwenye familia, jamii, serikali za mtaa, kitaifa na kimataifa.


Kushiriki katika kuandaa, kufuatilia na kutekeleza mikakati ya utendaji kazi kati ya Serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika na masuala ya watoto na jamii kwa ujumla katika kuleta mabadiliko yanayofaa kwa maendeleo ya mtoto.

 

Kukusanya maoni ya watoto wote Tanzania, kuyachambua na kuyawasilisha katika mamlaka husika na kuyafanyia kazi.

 

Kufanya kazi kwa karibú na Serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na taasisi zingine ikiwemo kuingia katika uwakala ili kutekeleza kwa ufanisi kazi za Baraza pale inapoonekana inafaa.

(Not translated)

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register