Log in
ELDERS FOR THE PREVENTION OF AIDS-UKIMWI

ELDERS FOR THE PREVENTION OF AIDS-UKIMWI

Masasi, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Baada ya kuwa kwa muda mrefu shughuli za asasi zilisimama,

sasa asasi imeanza tena shughuli zake. Wanachama wamekutana 

na kuazimia mambo kadhaa ya kuingia kwenye mpango wa mwaka

2016. 

Pamoja na kuwa kasi ya maambukizi ya ukimwi kuonekana kupungua lakini bado tatizo hili lipo ndani ya jamii.Ndiyo maana Epa-ukimwi imeanzisha jukwaa la wadau kupaza sauti na kuikumbusha jamii kuwa makini.Humo wanajamii wanaalikwa kushiriki katika kukemea matendo machafu na yanayohatarisha afya hasa kwa vijana.Siku za wanajukwaa kukutana ni Jumanne na ijumaa kila wiki.
Habari.Epa-ukimwi inawakaribisha wadau wapya katika Envaya kuwa na mawasiliano ya kupeana ushauri mawazo na usaidizi na asasi yetu.
Habari.Heri ya mwaka mpya wa 2015. Mwaka huu asasi yetu imekusudia kuendelea na mipango ya mwaka uliopita.Mipango na mikakati hii imelenga kuona kuwa jamii lengwa inapatiwa huduma stahiki.Hivyo ni wito wetu kwa wadau na wanaharakati wenzetu kutuunga mkono.Karibuni sana.

Asasi ya EPA-Ukimwi inakusudia kuanzisha vipindi vya utoaji elimu juu ya kutoa huduma kwa watu walioathirika na virusi vya ukimwi waweze kujizalishia mali kwa kutumia raslimali zinazopatikana ndani ya maeneo yao. Mafunzo haya yatakayohusisha washiriki 30 wa kata za Namajani na Mbonde-mtapika yataendeshwa na wawezeshaji ambao watatoka kwenye idara ya maendeleo ya jamii. Matarajio ni kuwa watakaopata mafunzo hayo wataondokana na hali ya utegemezi na kuweza kujikimu wao wenyewe na familia zao. Muda kamili bado haujaoangwa ila itakuwa kabla ya kipindi cha kilimo ili kuwawezesha washiriki kutoingilia ratiba zao za shughuli za kilimo.

Epa-ukimwi imefanikiwa kuwakutanisha watoa huduma majumbani wa kata 3 za mji wa Masasi na kuwapatia mafunzo ya rejea ya utoaji wa huduma kwa waathirika wa maambukizi ya virusi vya ukimwi. Hii ilifanywa ili kusaidia juhudi zinazofanywa na serikali kupitia kitengo cha CTC katika hospitali ya Mkomaindo.
Epa-ukimwi imeendesha kampeni ya kutembelea majando ya tohara za kienyeji ili kusaidia jamii kufuata maelekezo ya wataalamu. Maelekezo hayo ni pamoja na matumizi sahihi na salama ya vifaa vya kutahiria na matibabu. Majando yaliyopitiwa ni yale ya kata za Matawale, Mbonde na Temeke.

Jumla ya wanavikundi 20 wanaotoa huduma za wagonjwa majumbani

HBC attendants, wamepatiwa mafunzo ya rejea ya huduma zao

ili kuboresha stadi zao. Hii inafuatia mafunzo ya msingi waliyopatiwa

mnamo mwaka 2006. Ni matarajio ya asasi kuwa utendaji wao utaboreka

na kuleta manufaa kwa jamii wanazozihudumia.

Aasi yetu ya Epa ukimwi kwa kipindi cha June hadi July itakuwa inaendesha mafunzo ya awereness kwa makungwi na mangariba na manyakanga wa kata za Sululu, Mbonde na Namajani. Hiii ni kutokana na hitaji hilo katika kipindi hiki ambapo shughuli za unyago na jando ndiyo msimu wake. Jumla ya washiriki 33 wanatarajiwa kupatiwa mafunzo hayo na nyenzo za kuwasaidia.

habari ya mwaka mpya wa 2013. Nataraji mwaka huu mengi yatafanyika.