Envaya
Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

Asasi yetu ya Epa-ukimwi inakusudia kuzitumia sherehe za krismasi na mwaka mpya kama sehemu ya kufikisha ujumbe mpya wa kuitaka jamii kujitathmini toka kipindi cha sherehe zilizopita 2011 hadi sasa. Hii itasaidia jamii kuweza kuona ni kwa jinsi gani imeweza kushiriki katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya ukimwi. Sambamba na hilo kipindi hiki pia kitatumika kwa kutoa elimu kwa mangariba na manyakanga wanaosimamia taratibu na mila za tohara na unyago kwani kipindi hiki cha uvunaji wa korosho shughuli hizo hufanyika kwa kiwango kikubwa. Misaada mbalimbali toka kwa wadau wa asasi itahitajika katika kusukuma mbele jukumu hilo muhimu. Pia suala la kupitia katiba ya Tanzania linafanywa na wana asasi ili kutoa maoni yao na kuchangia katika mchakato wa marekebisho ya katiba unaoendelea hapa nchini.

Asasi ya EPA UKIMWI KWA KIPINDI CHA MIEZI MITATU YA AUGUST HADI NOVEMBER IMEKUWA IKIPITIA SHUGHULI ZAKE AMBAZO HAPO AWALI ZILIPATA USAIDIZI WA WAJISANI ILI KUONA UENDELEVU WAKE. BAADHI YA MIRADI IMESINZIA KUTOKANA NA JAMII KUPOTEZA BAADHI YA RASLIMALI WALIZOACHIWA ILI KUSAIDIA UTENDAJI WAO WA KILA SIKU. SEHEMU NYINGINE HALI YA UTEGEMEZI (MISAADA) IMEKWAMISHA UKAMILISHAJI WA MIRADI WALIYOJIWEKEA. HATA SEHEMU NYINGINE USIMAMIZI HAFIFU NDIYO SABABU. HIVYO KAMATI YA UTENDAJI INAPITIA TAARIFA HIZI ZOTE ILI KUWEZA KUANDAA PROGRAMU MPYA NA MIPANGO KAZI ITAKAYOWEZESHA KUHUISHA SHUGHULI HIZO KWA KUISHIRIKISHA JAMII HUSIKA, SERIKALI ZA MITAA NA VIJIJI. NI MATUMAINI YA UONGOZI KUWA HADI KUFIKIA DESEMBA BASI HAYO YATAKUWA YAMEFANYIKA NA MUNGU AKIPENDA JANUARI 2013 KUANZWE TENA SHUGHULI HIZO.

Mkakati wa sasa wa asasi yetu ni kuanza shughuli za utoaji tena ellimu kwa watoa huduma za wagonjwa majumbani na kwa watu wanaoendesha shughuli za jando na unyago. Hii ni kwa sababu kipindi hiki kwa mikoa ya kusini ya tanzania ya Mtwara na Lindi ni kipindi cha shughuli hizo za kimila. Hii itasaidia sana kuwafanya watoa huduma hao kuwa na uelewa na tahadhari katika shughuli zao. Miongoni mwa stadi zitakazowezeshwa ni; VVU katika Tanzania, Tohara na faida zake, kuepuka mafundisho yanayochochea vitendo vya ngono kwa wasichana wadogo na namna wazee wanavyopaswa kusikilizwa katika jamii. Wadau wengine watakaoshirikishwa ni viongozi wa kimila, viongozi wa kidini na washauri wa kijadi.

we thank the lord that we started this new year by having a members meeting which it discussed and approved the 2012 plan.  We also thank for our continuos solidarity. We promise all our stake holders to continue with our relationship.

Asasi ya Epa Ukimwi inaandaa warsha ya siku 6 itakayowahusisha wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya Ukimiw. Warsha hii itahusu kujadili mila na tanaduni zinazotumiwa na jamii bila yenyewe kujua kuwa iko katika hatari ya kupata maambukizi ya Ukimwi. Wahusika wakuu watakuwa ni wale ambao kwa namna moja wanahusika katika kuzitekelza mila na tamaduni hizo.

Aidha warsha pia itawaalika wataalamu mbalimbali watakaotoa mada zinazohusu maambukizi ya VVU na Ukimwi. Warsha hii itafanyika katika ofisi za Epa ukimwi maendeleo Masas kuanzia 15-21 Desemba 2011.

mojawapo wa watoto ambao EPA-UKIMWI imekuwa ikiwahudumia