Log in
Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) - Dodoma

Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) - Dodoma

Dodoma, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations
  1.     MALENGO YA CHAVITA

 

Kama wanajamii, viziwi wanayo haki ya kuchangamana na watu wengine na kushirikishwa  kikamilifu katika shughuli za jamii. Hii ni haki ya msingi ya binadamu. CHAVITA itahakikisha  hili kwa:

 

  • Kuhamasisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi popote walipo hapaTanzania, jamii ya watanzania, taasisi na serikali kuhusu haki za Viziwi.
  • Kupigania usawa katika fursa za elimu, huduma za jamii na nyanja zote za maisha ya binadamu.
  • Kupigania kutambulika kisheria kwa Lugha ya Alama yaTanzania.
  • Kujenga mwamko na kukuza matumizi ya Lugha ya Alama kwa matawi ya CHAVITA, jamii ya Viziwi nchini, na kwa jamii ya watanzania kwa ujumla.
  • Kuhakikisha shughuli za maendeleo ya jamii na ki-uchumi kwa matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini zinaboreshwa.
  • Kuhakikisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini wanapata uwakilishi katika ngazi zote za uongozi.
  • Kufanya na kuendeleza utafiti kuhusu masuala yanayowahusu Viziwi
  • Kupambana na Virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI pamoja na majanga mengine yanayowakabili Viziwi.
Latest Updates
Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) - Dodoma added a News update.
chavita tawi la mkoa wa Dodoma limezindua program ya mafunzo ya lugha za alama katika maeneo yafuatayo: UDOM, TCf, SAFINA KITUO CHA WATOTO YATIMA DOM na ST JOHN UNV DODOMA program hiyo ni ya miaka miwili kwa mujibu wa idara ya lugha ya alama chavita tawi la mkoa wa dom. mratibu wa mradi huo mr YUSUF MLOLI ambae ni... Read more
April 29, 2012
Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) - Dodoma added a News update.
Kesho Tarehe 11/02/2012 – saa 3:00 Mdahalo wa Wadau wa Maendeleo habari zaidi itakujia hivi punde...
February 10, 2012
Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) - Dodoma updated its Projects page.
Chavita ina Miradi miwili – Mradi wa Ushawishi na Utetezi kupunguza Umasikini kwa Viziwi Mkoa wa Dodoma – Mradi wa Lugha ya Alama kwa Wanachuo wa Chuo kikuu cha Udom
February 10, 2012
Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) - Dodoma updated its History page.
USULI – Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) ni chama kilichoanzishwa na Viziwi wenyewe mwaka 1983 na kusajiliwa rasmi na Wizara ya Mambo ya Ndani tarehe 04/09/1984 na kupewa no so. 6466 na baaada ya kupitishwa kwa sheria ya Uanzishwaji wa vyama vya kiraia... Read more
February 10, 2012
Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) - Dodoma updated its Team page.
Yusufu S. Mloli Mwenyekiti Pius Chiyenje Katibu Janeth thomas M/mwenyekiti Ismail M.Duru Mhazina Ally Jumanne Mjumbe K.K.U Mwendwa John Mjumbe... Read more
January 9, 2012
Other Websites
Sectors
Location
Dodoma, Tanzania
See nearby organizations