Log in
UTAWALA BORA KWA MAENDELEO (UBOMA)

UTAWALA BORA KWA MAENDELEO (UBOMA)

Kigoma Ujiji, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

MADHUMUNI NA KAZI ZA UBOMA

SERA

1. Kujenga ufahamu miongoni mwa jamii kuhusu umuhimu wa kushiriki katika uandaaji wa Sera mbalimbali za Taifa.

2. Kuikumbusha Serikali kuhusu haki ya wananchi kushirikishwa katika michakato mbalimbali ya Maendeleo ikiwa ni pamoja na Uandaaji na utekelezaji wa Sera mbalimbali.

3. Kuwashawishi na kuwawezesha wananchi kushiriki katika mchakato wa uandaaji na utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazowahusu.

4. Kufanya Utafiti na kuwapatia Taarifa wadau mbalimbali wa Maendeleo kuhusu Ushirikishwaji wa Jamii katika mchakato mzima wa uandaaji na utekelezaji wa Sera  na maendeleo ya Taifa

5. Kufanya Utafiti wa Utekelezaji wa Sera mbalimbali za Taifa kwa Ngazi ya Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa

UTAWALA BORA NA HAKI ZA BINADAMU

1. Kutoa Elimu ya Utawala Bora kwa jamii, Viongozi wa Serikali kuu na za Mitaa ili Dhana ya Demokrasia itafsiriwe kwa Vitendo na hivyo kufikia Maendeleo ya kweli.

2. Kuchapa Vitabu, Majarida na Magazeti yenye ujumbe wa Utawala Bora na Haki za Binadamu.

3. Kuainisha Uhusiano uliopo baina ya Utawala Bora na Haki za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi.

4. Kufanya Utafiti kuhusu hali halisi ya Utawala Bora na Haki za Binadamu kuanzia ngazi ya Uongozi kwa Sekta mbalimbali zinazohusika katika Usimamizi na Kutafsiri Sheria.

5. Kutoa Elimu ya Umuhimu wa Kumiliki Ardhi Kisheria kwa Wananchi na Wakulima ili waweze kupata dhamana mbalimbali ikiwamo Mikopo katika Taasisi za Fedha.

6. Kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Sheria katika kutoa Elimu ya Sheria na Haki za Binadamu kwa Jamii.