Fungua
UTAWALA BORA KWA MAENDELEO (UBOMA)

UTAWALA BORA KWA MAENDELEO (UBOMA)

Kigoma Ujiji, Tanzania

KUHUSU UBOMA.

Utawala Bora kwa Maendeleo (UBOMA) ni asasi isiyo ya kiserikali, isiyolenga kupata faida binafsi iliyoanzishwa mwaka 2009 na kusajiliwa Machi 26’ 2010 na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto kwa hati yenye namba OONGO 3798.

 UBOMA ilianzishwa kwa lengo la kupigania upatikanaji wa maendeleo endelevu kwa jamii ili kuona kwamba siku moja jamii ya kitanzania inaishi ikiwa bora katika kila sekta. Katika kulitimiza hili, Uboma ilifanya utafiti mdogo kuhusu wavuvi na maisha yao katika kata za Kibirizi na Katonga na haya hapa chini.

HALI IKOJE KIBIRIZI NA KATONGA?

Wakazi wa Kibirizi na Katonga ni miongoni mwa wananchi wengi masikini wa mkoa wa Kigoma wanaoishi chini ya dola moja kwa siku. Licha ya kujishughulisha na uvuvi na           kuzungukwa na Ziwa Tanganyika lenye Samaki, Dagaa na rasilimali anuai ambazo ni malighafi adhimu na inayohitajika kote       Tanzania na nchi za nje; bado wengi wao     wameendelea kuishi katika lindi la             umasikini wakikabiliwa na ukosefu wa huduma bora za Afya, Elimu bora na miundombinu duni ya umeme maji na barabara.

Pamoja na hali hii, wananchi hawa wamekuwa wakichangia pato la taifa kupitia kodi na ushuru wa bidhaa kila wanapotoka ziwani   kuvua samaki au dagaa. Wakati mwingine   hulilipa hata jeshi la Ulinzi la Tanzania (JWTZ) kiasi cha Tsh 10,000 kila mwezi ili   liwalinde na majambazi wanapokuwa katika uvuvi     Ziwani nyakati za usiku! Hili ni jambo la ajabu kwa kuwa jeshi linaendeshwa kwa kodi za   watanzania na Ulinzi ni jukumu lake la msingi.

 

Katika uchunguzi wake UBOMA imefanikiwa kuongea na wavuvi kadhaa wa Kibirizi na     Katonga kuhusu jinsi wanavyoshirikishwa katika mipango mbalimbali ya maendeleo ya kijamii katika kata zao na ile ya kuboresha sekta ya Uvuvi, aidha kama wanafahamu haki yao ya kushiriki katika   upangaji wa         viwango vya ushuru kisha kupatiwa taarifa ya                 makusanyo na matumizi na mamlaka         zinazohusika (Halmashauri). Jibu lilikuwa     hapana.

 

Wavuvi wote waliohojiwa wameeleza       kutofahamu na kwamba wanachojua serikali wanakusanya fedha zao kwa ajili ya   uendeshaji wa shughuli mbalimbali za     kiserikali. Hali hii ndiyo iliyoisukuma UBOMA kuandaa Mafunzo ya Usimamizi wa         Rasilimali za sekta ya uvuvi kwa wavuvi na wadau muhimu wa sekta hii ili kuhakikisha           zinawanufaisha na hivyo kuinua uchumi wa jamii ya wavuvi ikiwa ni pamoja na kuboreshwa kwa huduma za kijamii.