DIRA
Dira ya Baraza ni kuwa chombo imara cha kutetea haki za watoto na kuhamasisha Utekelezaji wa haki hizo na kuelimisha watoto na jamii kuhusu haki na wajibu wa mtoto ili kujenga Tanzania bora na dunia imfaayo kila mtoto.
DHIMA
Dhima ya Baraza ni kuwaunganisha na kuwajenga watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mazingira bora ya kidemokrasia na kupata uzoefu wa kushiriki na kushirikishwa kikamilifu katika uwakilishi katika michakato mbalimbai ya kisera na ufanyaji maamuzi ili kulinda na kutetea ipasavyo haki na maslahi ya mtoto ili kufikia azma ya kuwa na Tanzania na dunia imfaayo kila mtoto ili kuwezesha watoto kulelewa vema na kufikia upeo wa uwezo wao kiakili, kiafya, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.
MALENGO
Baraza la Watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litakuwa na madhumuni yafuatayo:-
Kutoa fursa kwa watoto kusikika kupitia mikutano ya kitaifa na kimataifa ya majadiliano kuhusiana na masuala yanayowahusu watoto.
Kujenga ushirikiano wa karibu kati na baina ya watoto, vyombo vya habari, mashirika yasiyo ya kiserikali na Serikali.
Kuhakikisha watoto wanapata habari na taarifa sahihi zinazowahusu.
Kufuatilia utekelezaji wa sera na sheria mbalimbali za nchi zinazowahusu watoto.
Kuelimisha jamii na watoto juu ya haki na wajibu wa mtoto.
Kushiriki kwenye harakati za watoto duniani na ufuatiliaji wa mikakati ya Azimio la ‘Dunia Iwafaayo Watoto’.
Kujenga uhusiano na ushirikiano na Mabaraza na Mabunge mbalimbali ya watoto duniani.
Kukuza na kubadilishana uzoefu na ujuzi na Mabaraza na Mabunge mengine ya watoto duniani katika kupigania haki, wajibu na maendeleo ya mtoto.
Kutetea haki za watoto na maslahi ya watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Latest Updates

Baraza la Watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania added 3 News updates.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto wa Taifa akifanya mahojiano na Mh. Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ndg. Pindi Chana mara baada ya hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Baraza la Watoto wa Taifa Read more
March 12, 2014

Baraza la Watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania added 4 News updates.
Baraza la Watoto wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mlisho Kikwete mwaka 2010, ikulu Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuzungumza nae kuhusu Ajenda ya watoto Read more
March 7, 2014
Baraza la Watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania updated its Team page.
Baraza la Watoto linamfumo ufuatao wa Uongozi – Kamati Kuu – Mwenyekiti.... Read more
March 7, 2014

Baraza la Watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania created a Projects page.
Baraza la Watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunafanya kazi zifuatazo: – Kutayarisha mikakati ya kukuza ushirikishwaji wa watoto kwenye mambo yanayowahusu watoto katika ngazi zote kuanzia kwenye familia, jamii,... Read more
March 7, 2014
Baraza la Watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania updated its History page.
Baraza la Watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina historia inayoanzia katika Mkutano wa watoto kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania bara na visiwani waliokutana katika mkutano wa maandalizi ya Mkutano Maalum wa Baraza la Umoja wa Mataifakuhusu watoto uliofanyika tarehe 8-10 Mei 2002. Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa hukutanisha... Read more
March 7, 2014
Sectors
Location
Dar es Salaam, Tanzania
See nearby organizations
See nearby organizations