Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Sababu kuu nne ‘zinazowatafuna’ wakulima wa korosho nchini.

 

MKOA wa Mtwara umezungukwa na Bahari ya Hindi, na eneo la nchi kavu kuna miti ya mikorosho iliyopandwa tangu enzi ya wakoloni.

Ni moja ya mikoa nchini inayowavutia watu wengi wakiwamo wawekezaji,  hasa baada ya Serikali kuanza kuchimba gesi na kubadilisha mfumo wa kuuza zao la korosho na kuwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani.

Korosho ndilo zao kuu la biashara katika mikoa ya Pwani, Lindi, Ruvuma na Mtwara.

Kwa Mtwara,  mkoa huo umekuwa maarufu zaidi baada ya wataalamu kueleza kwamba panapochimbwa gesi pia mafuta yanapatikana.

Ndiyo maana hivi sasa ukifika katika mkoa huo,  moja ya mambo yanayozungumzwa na wananchi, ni gesi kuhamishiwa mkoani Dar es Salaam na kuyumba kwa soko la korosho nchini.

Msingi wa makala haya ni kuzungumzia mambo yanayosababisha kuyumba kwa soko la korosho. Kwa mfano, makala haya yanauliza, Kwa nini soko la korosho linayumba?

Baadhi ya wakulima katika wilaya za mkoa huo  kwa nyakati tofauti,  wanasema soko la korosho linayumba kwa sababu mfumo wa stakabadhi ghalani umeingiliwa na watu wanaosimamia maslahi yao badala ya wakulima.

Wanasema mambo yanayosababisha kuyumba kwa zao la korosho ni vyama vya msingi kutokuwa na mtaji wa kununua korosho kutoka kwa wakulima, baadhi ya wafanyakazi wa serikali kuhusika kuwakandamiza wakulima, mgomo baridi wa wafanyabiashara na madeni kutoka vyama vya msingi.

Sababu hizo zimechangia wakulima wa korosho kutonufaika na kilimo hicho, na pia kusuasua kwa vyama vya ushirika ambavyo havina  mtaji kwani navyo vinategemea fedha kutoka kwa wakulima hao

Kwa mfano, chama cha ushirika cha msingi cha wilaya kinachukua Sh50 katika kila kilo moja ya mkulima ikiwa ni gharama za uendeshaji.

Katika makato ya Sh50 kwa kila kilo, msimu wa korosho mwaka wa mwaka jana (2011/2012) wilaya ya Newala na Tandahimba waliuza kilo 64, 124, 110 kwa wanunuzi na kupata jumla ya Sh76.5 bilioni.

Kwa hoja hiyo ikiwa utazidisha kilo za wilaya hizo zilizouzwa kwa Sh50, hakika vyama vya ushirika vilikusanya fedha nyingi.

January 11, 2013
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.