Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

BABA ABAKA MWANAE WA MIAKA 2.5 NA KUMUUMIZA VIBAYA.

WAKATI wanaharakati wakipaza sauti za siku 16 za kupinga ukatili
,mkazi mmoja wa mtaa wa Sedeko kata ya Stendi kuu wilayani Serengeti
John Nashon(25)amembaka mwanae wa miaka 2.5 na kumuumiza vibaya kisha
akatoroka.

Tukio hilo ambalo limepokelewa kwa hisia tofauti na wakazi wa mji wa
Mugumu linadaiwa kutokea novemba 26,majira ya saa 12.00 jioni mwaka
huu katika mtaa huo na kuripotiwa kituo cha polisi Mugumu mjini.

Mama mzazi wa mtoto huyo akiongea na Mwananchi akiwa hospitali teule
ya Nyerere ddh alikolazwa kitanda namba 8 wodi ya watoto ,alisema
wakati unyama huo unatendeka alikuwa sokoni.

“Nilimwacha mwanangu na baba yake ambaye ni fundi wa magari gereji ya
Mayala mjini hapa,kurudi kufika mlangoni mme wangu akanieleza niingie
ndani haraka nimkande mtoto mwili mzima kwa maji baridi…nilikuwa sijui
kinachoendelea”alisema na kuendelea

“Kuingia chumba cha kulala nikamkuta mtoto amelala
kitandani,kumnyanyua damu zikamwagika mithili ya maji kutoka sehemu
yake ya siri…kumwangalia nikakuta amechanika sehemu zake za
siri”alisema.

Hali hiyo ilimpelekea kumwangukia mwanae na kuanza kulia kwa uchungu
na alipotaka maelezo kwa mme wake alisema alimsukuma kwa bahati mbaya
mwanae akaanguka kwenye kochi na kuchomwa na msumari sehemu zake za
siri.

“Nilipomwambia tumpeleke hospitali akakataa tena akinitishia kunipiga
kwa madai kuwa siri itafichuka…niligundua kumbe ndiye kafanya unyama
huo,nilitoka kwa nguvu hadi kituo cha polisi na kupewa pf 3,nikimwacha
hapo,lakini alikimbia na haijulikani alipo”alisema.

Hata hivyo alipomuuliza mwanae kilichomtokea akasema kuwa baba yake
ndiye aliyemfanyia unyama,huku akishangaa kwa kitendo hicho kwenye
ndoa yao iliyodumu kwa mwaka mmoja toka novemba 2011.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo Dk.Kelvin Mwasha amekiri kumpokea mtoto
huyo na kuwa amelazwa wodi la watoto ,kutokana na maumivu na kuvuja
damu nyingi ililazimu kuongezewa damu.

“Sehemu zake za siri zilikutwa zimeharibiwa sana ,amepata huduma ikiwa
ni pamoja na kuchukua sampuli za maji yaliyokuwa yanatoka ukeni kwa
ajili ya vipimo …amekutwa yuko salama,lakini hili tukio si la kawaida
linatakiwa kulaaniwa ,na ndiyo yanaifanya wilaya kuonekana na matukio
ya ukatili”alisema.

Hivi karibuni katika uzinduzi wa siku 16 zakupinga ukatili kamanda wa
polisi mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma alisema kunaongezeko kubwa la
matukio ya ukatili,ambapo kwa mwaka huu toka januari yameripotiwa
matukio 201 ikiwa ni tofauti na mwaka 2011 matukio 148 yaliriripotiwa
polisi.

Mwisho.



November 28, 2012
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.