Envaya
Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

large.jpg

FEMALE CONDOM DEMONSTRATION

UVIKITWE GROUP, kupitia ufadhili wa The Foundation For Civil Society, imefanikiwa kutekeleza mradi  wa uelimishajirika kwa vijana kuhusu athari za matumizi ya dawa za kulevya na uhusiano wake na maambukizi ya VVU/UKIMWI. Mradi huu umetekalezwa katika wilaya ya Bagamoyo  ndani ya kata sita ambazo ni Vigwaza,Chalinze,Ubena,Msata,Miono na Kiwangwa. Mradi huu umeweza kuwafikia vijana tisini (90) wanaotumia na wasiotumia dawa za kulevya.

Mafanikio ya mradi

  • Kuanzishwa na kusajiliwa kwa CBOs  kumi (10) zinazo toa elimu hii kwa jamii.
  • Vijana wapatao  12  waliokuwa wanatumia dawa za kulevya , wameweza kujitambua na kuachamatumizi ya dawa za kulevya
  • Vijana wanne  4 wameweza kuteuliwa na kuingia kwenye kamati za ukimwi za kata na kuwakilsha kwenye kamati za WODC ngazi ya kata

Changamoto tulizokutana nazo.

  • Mahitaji  ya jamii husika kuwa juu kuliko uwezo wa taasisi
  • Uhitaji wa elimu ya stadi za maisha kwa jamii yote, kama nyenzo ya kuleta mabadiliko ya tabia.
  • Wilaya ya Bagamoyo kuwa njia kuu ya kuingiza dawa za kulevya kutoka  Zanzibara, ambako ndiyo njia kuu ya kuingizia dawa za kulevya kutoka nchi za nje.B

 

 

 

 

 

 

Picha za baadhi ya vijana wa kata za mradi waliohudhuria mafunzo ya elimurika kuhusu athari za matumizi ya dawa za kulevya  na uhusiano wake na maambukizi ya VVU/UKIMWI.

large.jpg

Majadiliano katika maeneo ya wazi na wananci wanaoishi kwenye machimbo ya Masuguru Mbinga

large.jpg

Baadhi ya akina dada waliokuwa wanafanya biashara ya ngono katika machimbo wilayani Mbinga wakiwa pamoja na uongozi wa Uvikitwe katika ofisi za kata ya Kigonsera Mbinga

Mradi wa elimu ya kina kuhusu uwezo kujikinga na maambukizi ya VVU/UKIMWI kwa wafanya biashara za ngono na watumiaji wa dawa za kulevya katika maeneo ya machimbo ya Dar-pori, Masuguru, Mpepo na Lukarasi yalioko katika wilaya ya Mbinga - mkoa wa Ruvuma. Mradi huu umeweza kuleta mabadiliko makubwa sana kwa wlengwa wa moja kwa moja, baada ya kupewa elimu ya stadi za maisha na kuweza kuwajengea uwezo wa kujitambua na kutambua mahitaji yao ya msingi, pia mradi huu umeweza kuleta mabadiliko ya shughuli za kiuchumi hasa kwa akina dada wanaojiuza kwenye maeneo ya ya machimbo baaday kuwa kufikia uamuzi wa kubadilisha kazi ya kujiuza kama njia ya kijipatia riziki ya kilasiku, na kuanzisha biashara zingine kwa mtaji wa sh millioni 25 ( TZS 25,000,000) kama ruzuku kwa njia ya vikundi. vikundi vilivyoanzishwa na kusajiliwa rasimi na serikali ni vikundi 12, kumi vikiwa ni vya akina dada na viwili ni vya akina kaka wanaotumia dawa za kulevya. Lengo la uvikitwe ni kuweza kutumia fursa zilizopo ili kuweza kuiokoa jamii ya kitanzania hasa iliokuwa masikini zaidi, kwa kuwajengea uwezo wa kiuchumi, kiutamaduni na kisikolojia.