Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Kutokana nakutokuwa hewani kwa muda mrefu Tunaweza Women Group tunaomba radhi kwani ilikuwa nje ya uwezo wetu, napenda kuwajulisha kuwa hivi sasa tumerudi tena natunaendelea na kazi za kulijenga taifa letu shime wana Azaki tushirikiane

Ahsante wenu katika ujenzi wa taifa

Ariziki Mtambalike

Baada ya kumaliza mafunzo yaliyo tuwezesha  kuelewa na kuandika mpango mkakati, kanuni na utunzaji wa fedha za asasi, tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa uongozi na wafanya kazi wote wa The foundation for civil sociaty kwa kuweza kutuwezesha kufika hapa tulipo.

Pamoja nashukrani hizo pia tunatoa shukrani kwenu shirika la Envaya kwa kutuwezesha kusikika na kubadilishana mawazo na wadauwenzetu, tunaomba kuwakumbusha ombi letu lawafanya kazi wa kujitolea bado tunasubiri na hivi sasa ndo tunawahitaji sana kwani kazi zimeongezeka katika shirika kulingana na mpango mkakati tulio nao.

Ndugu  wadau pamoja na wana asasi wote natumaini wote hamjambo pamoja nakuwa wote tuko ndani ya chombo kimoja au boti moja nia na madhumuni nikupata ulimengu wenye usawa na haki maridhawa  amani na utulivu.Pamoja nakuwa ndani ya chombo kimoja lakini milango ya kutokea ni tofauti sisi wenzenu wana TUNAWEZA WOMEN GROUP tume azimia kutoa chagamoto kwa  wanafunzi wa shule za msingi hapa nchini tukianzia na manispaa ya ilala

Changa moto yenyewe ni kwamba tuna azimia kutoa zawadi kwa wanafunzi watakao fanya vizuri katika mitihani yao ya kila mwisho wa muhula tumekusudia kutoa zawadi kwa wanafunzi watakao shika nafasi ya kwnza mpaka nafasi ya kumi tunatarajia zawadi hizi zitaongeza nguvu najuhudi ya kujisomea kwa wanafunzi kuanzia madarasa ya chini.

Hivyo basi ilikufanikisha zoezi hili tunawaomba wadau wote mtusaide michango yenu ili kusudio letu litimie tunapokea michango ya pesa au vifaa vya shule 

Natanguliza shukran kwenu naomba ushirikiano kwa mawasiliano

A.Mtambalike

k.n mwenye kiti

0784 399400

 

Tunatoa shukrani kubwa kwa shirika la The foundation for civil society kwa kutuwezesha kupata mafunzo ya uongozi mpango mkakati pamoja na utunzaji wa fedha kwani japo kuwa tuli anza kukata tamaa kwa kuchelewa kwa ruzuku hivi sasa tuna fanya kazi kwa kujiamini japokuwa bado tunaendelea na mafunzo . 

vijana wamekuwa na muamko mkubwa wa mafunzo ya uelimishaji rika yanayo tolewa na shirika kila juma mosi mafanikio ya kuwapata vijana wengi yamepatikana, shirika lilipo anzisha michezo mbalimbali hasa mpira wa miguu kwa vijana walioko mashuleni na walio maliza masomo wa rika tofauti lengo lashirika kuwaepusha vijana namakundi ya kuwapotosha,makundi ya ulevi n.k