Baada ya tovuti ya asasi yako kupitishwa na Envaya, mtu yeyote akiwa kwenye mtandao atakuwa na uwezo wa kuona tovuti yako bila kuhitaji kujiandikisha Envaya.
Hata hivyo, ni wewe tu (na mtu yeyote ambaye anajua jina la mtumiaji na neno la siri la asasi yako) mnaweza kuhariri ukurasa kwenye tovuti yenu kama umeingia kwenye tovuti ya Envaya.
Kwa kuangalia rangi ya ukurasa, unaweza kujua kama ukurasa unaonekana na kila mmoja au unaweza kuona wewe mwenyewe tu unapoingia kwenye akaunti yako ya Envaya.Kurasa zenye rangi ya kijivu zinapatikana tu wakati umeingia kwenye akaunti yako.
Unapojisajiri Envaya kwa mara ya kwanza, moja kwa moja utakuwa umeingia kwenye akauti yako ya Envaya. Ukiwa umeingia kwenye akaunti yako, utaona sehemu ya bluu upande wa kulia juu yenye vipengele kama inavyoonekana hapa chini:

Kila kipengele utakachobonyeza kitakupeleka kwenye ukurasa mwingine:
Ni ukurasa mkuu wa akaunti yako.
Ni ukurasa wa kuhariri, ambapo unaweza kuchapisha habari na picha, kuchapisha mabadiliko na kuhariri ukurasa wowote kwenye tovuti yako.
Inatumika kufanyia marekebisho katika akaunti yako ya Envaya, ambapo unaweza kuchapisha upya taarifa zako za mawasiliano ya asasi yako na marekebisho mengine.
Ni kipengele cha kuondoka kwenye akaunti yako ya Envaya.
mahali kuu ya kuhariri tovuti yako ni sehemu iliyoandikwa Hariri Tovuti. Katika ukurasa huu, unaweza kuandika mabadiliko mapya na kuhariri ukurasa wowote kwenye tovuti yako. Wakati umeingia, mara nyingi unaweza kupata ukurasa huu kwa kubonyeza kitufe
Kujifunza jinsi ya kufanya kazi maalum kwenye tovuti yako, chagua sehemu kutoka kwenye orodha hapo chini.