| Base (Swahili) | Kinyarwanda |
|---|---|
|
Jamii ya Viziwi tunadharauliwa kwa kutuita sisi Mabubu, Maana ya Neno BUBU? Jamii ya watu wanaosikia hawajui Maana ya Bubu neno ilo ni Dharau kubwa sana na Ni kosa kulitamka.Viziwi hawataki kuitwa Bubu labda sema Mlemavu wa Masikio au KIZIWI au Hasikii,Viziwi wana Lugha maalum ya Mawasiliano kwa kutumia Viganja vya mikono yao na Vidole ndo wanaongea kwa ishara za maana sana. Aidha Jamii ya walemavu wengine hatuna tofauti na dharau za Viziwi na wao wanadharauliwa kwa kuitwa majina kama Maalbino wanaita ZERUZERU,VIWETE,VIPOVU badala ya Lugha nzuri ya Wasioona,Walemavu wa Viungo n.k |
(Not translated) |