Base (Swahili) | English |
---|---|
Shirika letu kwa sasa tumeweza kuwasaidia watoto 45 wanaoishi katika mazingira hatarishi wa vijiji vya Lusanga, Kwadoli na Dihinda kupunguza makali ya maisha kwa kuwapatia chakula,nguo na vifaa vya kusomea. Pia upande wa VVU/UKIMWI shirika limeweza kuendesha zoezi la kupima kwa hiari katika kijiji cha Lusanga ili kubaini maambukizi mapya hapo mwaka 2009 na 2010 na kubaini waathirika 18 ambao wanapata huduma ya dawa za kurefusha maisha sasa. ELIMU:Shirika limeendelea kutoa elimu ya tekinolojia kwa vijana na watu wazima chini ya mradi wake wa ongeza maarifa ya tekinohama(omayate), mpaka sasa vijana 17 na watu wazima 10 wamepata elimu ya tekinohama,mradi huu ulianza mwezi wa July 2010 na ni mradi endelevu. Shirika linakusudia kuendesha mradi wa kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji katika Tarafa 2 za Turiani na Mvomero hapo ifikapo June 2011 kama tutapata ufadhili mapema. |
Our organization for now we can help 45 children living in vulnerable villages Lusanga, Kwadoli and Dihinda cutting edge of life by providing food, clothes and study materials. Also on the HIV / AIDS organization has been able to operate freely exercise testing in the village of Lusanga to identify new infections there in 2009 and 2010 to identify 18 victims who have access to antiretroviral treatment now. EDUCATION: The organization developed to provide education to technology for youth and adults under the project of the added knowledge of tekinohama (omayate), until now a young 17 and adults 10 have received education tekinohama, this project began in the month of July 2010 and is a sustainable program . Organization project to reduce operating linakusudia conflict with farmers and pastoralists in Division 2 and Mvomero Turiani there by June 2011 if we get funding early. |
Translation History
|