Base (Swahili) | English |
---|---|
Katika mwezi wa kwanza hadi mwezi wa tatu mwaka 2014 Asasi ya jinsia na maendeleo rombo imeweza kuendesha mafunzo ya wanawake na uongozi mradi ambao umefadhiliwa na The foundation for civil society. Kutokana na uendeshaji wa mafunzo haya yameweza kuleta mabadiliko makubwa kwa wanawake katika nyanja ya uongozi ambao umewawezesha kufanya utetezi ambao umegawanyika katika sehemu kuu zifuatazo:-
Shirika la AJIMARO likishirikiana na mfadhili wake The foundation for civil society wameshiriki kikamilifu katika mchako huu wa utoaji wa mafunzo ya uongozi na ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi kwa kuwawezesha vikundi vya wanawake toka kata zifuatazo:Ubetu/kahe
Mafunzo haya yamesaidia wanawake kutokuwa nyuma katika masuala mbalimbali: I. Kugombea uongozi na kuingia katika vyombo vya maamuzi II. Upatikanaji wa habari muhimu zinazosaidia katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazomuhusu mwanamke
AJIMARO kwa kushirikiana na wawezeshaji wameweza kugawa vitini vya uongozi kwa washiriki ili uwe muongozo utakaowawezesha kutoa mafunzo hayo kwa wanawake wengine. Kitini hicho ni mahususi kumsaidia mwanamke ambae anania ya dhati katika kumkomboa mwanamke kwa kuwapa elimu ambao yeye ameipata katika mafunzo haya. Kitini hicho kimeelezea matamko mbalimbali na kutambua dhana nzima ya uongozi pia kujua haki zao kutokana na katiba ya jamuhuri wa muungano wa Tanzania (kifungu cha tatu)inalinda uhuru wa mtu mwanamke au mwanaume kupata hifadhi ya maisha,kumiliki mali na pato la jasho lake, kufanya kazi na kupata haki ya kujielimisha kufikia upeo wake.kwa kifupi kutokana na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Sera ya taifa ya maendeleo ya wanawake jinsia na watoto ya mwaka 2000 na shirika letu la AJIMARO inataka kuwepo kwa jamii yenye usawa,haki |
(Not translated) |