Base (English) | English |
---|---|
Blue Star Media Blue Star Media ni Asasi isiyo ya Kiserikali iliyoanzishwa mwaka 2016 ambayo inajishughulisha na masuala ya uandaaji Sinema (Movie) pamoja na video mbalimbali. Pia inajishughulisha na masuala ya kutoa mafunzo kwa wasanii mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine badi wanahitaji kuongezewa taaluma hiyo ya sanaa. Katika kukuza vipaji, Asasi hii ina uwezo wa kutoa mafunzo kwa watoto wadogo ambao mara nyingi ama wazazi wao au walezi wao huwa wanakosa muda wa kuwaangalia na kugundua uwezo wa watoto wao katika suala zima la vipaji. Aidha, Asasi hii itajihusisha katika suala la kusaidia watoto yatima pamoja na walemavu kupitia sanaa na maonesho. Hii ni baada ya kuona kuwa Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina mzigo mkubwa wa kimaendeleo, hivyo si vibaya asasi ikatumia mwanya huo kuisaidia katika hili. Imeandaliwa na: Hamis Namawala. Mwenyekiti. |
(Not translated) |