Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
Taarifa ya mafunzo ya stadi za maisha na uongozi yaliyotolewa kwa VSI katika ukumbi wa ofisi ya WOY Moshi Utangulizi Kwa msaada kutoka SATF White Orange Youth wanatekeleza mradi unaitwa ‘Vijana Simam Imara’ Mradi huu umeanzishwa kwa kujifunza mafanikio ya mfano kwa shirika la Humuliza linalopatikana kanda ya ziwa Victoria. Shughuli ambazo WOY wanafanya katika mradi huu ni pamoja na kuwafundisha vijana elimu ya uongozi na stadi za maisha Katika mwezi wa Mei WOY ilifanya mafunzo ya Stadi za maisha na Uongozi kwa VSI. Mafunzo haya yalifanyika kwa muda wa siku tatu ambapo jumla ya watoto 26 waliudhuria. Mafunzo haya yalifanyika katika ofisi za WOY zilizopo majengo. Malengo ya Mafunzo Washiriki wa mafunzo haya walielezwa kuwa baada ya mafunzo wataweza kufahamu yafuatayo: • Kueleza maana ya stadi za maisha • Kuorodhesha mahitaji ya stadi ya stadi za maisha kufuatana na maarifa, mitazamo na vitendo • Kufafanua aina za stadi za maisha • Kutambua umuhimu wa stadi za maisha Mwezashaji alielezea kwamba stadi za maisha ni uwezo wa kutumia maarifa na ujuzi, vitendo, mitazamo, na tabia zinazomweka mtu katika katika hali ya maisha ya siku ili kuweza kumudu mazingira mbalimbali yanayomkabili. Mwezeshaji pia alielezea pia kuhusu mahitaji ya stadi za maisha katika maarifa, vitendo na mikazo kama ifuatavyo Maarifa -Vyanzo vya ushauri na taarifa za kisheria -Vyanzo vya huduma na elimu ya afya -Haki ya na majukumu ya binaadamu -Aina ya mahusiano kati ya familia na na wanarika -Maisha na afya bora -Mabadiiko na makuzi ya binaadamu -Usawa wa kijinsia -Mahusiano ya mitindo ya maisha -Mahitaji binafsi Mitizamo -Kujitambua -Ustaimilivu -Kuheshimu mwenendo wa kisheria -Kujiheshimu -Kuwajibika -Kujiamini -Uvumilivu -Kuthaminin mawazo na hisia za wengine - Kujali Vitendo Kuweka maengo na kutekeleza mipango Kutafuta msaada Kumudu kwa ufanisi na ukakakmavu wa mazingira mapya Kutoa na kutekeleza maamuzi Uwezo wa kuwasialiana Kutenda kwa busara Makundi ya stadi za maisha yalifafanuliwa kama ifuatavyo 1. Stadi za kujitambua binafsi: Ilielezewa kuwa kijana anaitajika kujitambua, kujifahama, kujithamini na kujiamini 2. Sati za kufahamana kukuwezesha kuishi nawatu wengine: Kuhusiana na stadi hii, ilielezewa kuwa mahusiano mazuri baina ya mtu mmoja na mwingine ni muhimu, pia ushirikeli, ushupavu, uwezo wa kustahimi;I shinnikizo , msongo na mhemuko, pia mawasiliano yenye ufanisi baina ya vijana ni jambo muhimu maishani. Kujitambua na kujifahamu Ilielezewa kuwa huu ni uwezo wa kujielewa mwenyewe yakwamba inahusisha kutambua uwezo wa hisia zako, tabia na mwenendo, mihemko kufuatana na mahali unapotoka, mila, desturi pia mabo usiyotegemea kuyafanya maishani mwako. Maswali ya kujiuliza 1 Mimi ni nani? 2 Ni vitu gani ninavyothamini? 3 Jamii inategemea nini kutoka kwangu? Mwezeshaji aliwaeleza washiriki faida za kujitambua kama ifuatavyo 1 Kujiwekea malengo 2 Kujikinga katika matatizo mbalimbali kwa mfano, kukamatwa kwa wiai, kupata mimba za utotoni, kuambukizwa virusi vya ukimwi nk 3. Kukubalika na kueshimika 4. Kuondoa matatizo kwa kumwelewa mtu 5. Kujiweka katika mweekeo mzuri wa maisha Kujithamini na kujiamini Ilielezwa kuwa hizi ni hisia za binafsi, kuwa na uhakika na kujiwekea au kujionyesha kwa watu wengine katika kufanya kitu bora kikaeshimika na kupendwa. Pia hii inatokana na mtu mwenyewe anavyojiona, uwezo wake, malengo yake, mwenendo wake na mafanikio yake kwa ujumla. Katika stadi hii mwezeshaji alielezea faida zake kama ifuatavyo 1 inawezesha kufanya maamuzi ya busara kuhusu afya yako 2 Vijana lazima wawe na uwezo wa kuweza kujibu maswali wao binafsi kuingana na wanachofikiria ni kizuri kwao 3 Vijan watakuwa nauwezo wa kusema HAPANA kwani huonyesha ni jinsi gani anavyojiamini . kukataa jambo ambalo alitaki mbele ya wenzake na hayupo tayari kufuata mikumbu. Vilevile kuheshimu uamuzi wa mtu aliyesema hapana inaonyesha anajali nafsi yake. Stadi za kufahamu na kuishi na wengine Mahusiano Iielezewa kuwa huu ni uwezo wa kukutana na kufaamiana na watu wengine na watu wengine katika makusanyiko tofauti na watu wengine katika jamii, shueni , michezonin na mahali pa kazi. Ilielezewa pia watu wanaweza kukubaliana kutokana na mtazamo au mienendo inayofanana. Hatari za mahusiano ya kijinsia kati vijana wa kiume Ufafanuzi ulitolewa kuwa mahali penye wavulana na wasichana lazima kuna mahusiano na yanaweza kupelekea kwenye urafiki wa kawaida au wakimapenzi ambapo uhusianao wa kimapenzi unaweza kusababisha yafuatayo 1 Mimba zisizotarajiwa 2 Utowaji wa mimba 3 magonjwa yatokanayo na kujamiiana na UKIMWI Vijana wanapaswa kujihadhari na kujiaandaa kutatua matataizo yao Uhusiano wa kimapenzi hauwezi kuwepo bila mapenzi Lakini watu wanaweza kupendana bila kujamiana Ushirikeli - Ni mahusiano katika kukuza, kujali na kuwa makini katika matakwa binafsi - Ni uwezo wa kujiweka katika hisia za watu wengine - Stadi hii inatusaidia katika kukuza mahusiano ya kuishai pamoja kwa furaha kadhalika kukubali jambo bila kuwa na uzoefu nao Kustahimili Shinikizo -Ilielezewa kuwa huu ni uwezo wa kuwa na msimamo wa kuwa na amani, imani na mitizamo binafsi, uwezo wa kukataa au kukubai shinikizo rika - Inahitaji ushupavu na ujasiri kwani unaweza kuhatarisha mahusiana mahusiano na wanarika wengine - Stadi za kuweza kukataa na kusisitiza ni muhimu sana kwa vijana Kustahimili Mihemuko Ilielezewa kwamba huu ni uwezo wa kustahimili mhemuko kutokana na hasira, mshtuko, penzi na mchomo wa mojo unaogusa hisia. Hali hizi zinadhuru mwenendo na tabia na zinaweza kusababisha matendo yasiyotabirika na yakusikitisha. Hisia zinazojionyeshakatika mhemuko - Huzuni, hasira, Hofu, shauhuku, mkanganyiko upendo, Hisia kali, maumivu , maudhi , majonzi, majuto, wivu, furaha, kicheko. Kustahimili msongo Mwezeshaji alielezea kuwa msongo ni yale mabo mengi yanayotuandama katika maisha yetu kwa mfano shinikizo la kazi, kifo cha rafiki, kunyimwa haki, kukataliwa na mchumba -kulaumiwa kila wakati, nk Huu unaweza kuathiri mwenendo na tabia na unaweza ukawa ni chanzo cha uharibifu na ghasia kwa kufanya maamuzi mabaya kama ulezi na nk. Stadi za mawasiliano Ilielezewa kwamba kuwasiana ni jambo muhimu katika kuelewanana na kwamba uwezi kufikia malengo yako kama hauna mbinu za kuwasiliana unaweza usieleweke. Unapomweleza mtu jambo au unapomjibu mtu jambo aelewe nachokusudia. Hata akuelewe unavyotaka akuelewe. Kutokueleweka kunaweza kukuingiza kwenye janga. Kufanya uamuzi sahii -Ni uwezo wa kutoa uamuzi au kuchangia lilio bora katika uchaguzi kadhaa zilizopata kufikiriwa kwa makini na kwa ubunifu -Uamuzi sahii ni ule unaoweza kutekeleza na usio na madhara katika maisha Umuhimu wa stadi za maisha. Ilielezewa kuwa inakuza mienendo na tabia njema kama, tabia ya uwajibikaji katika mapenzi zinapunguza ugomvi. - Zinaongeza uhusiano kati ya vijana na watu wazima Athari za kutotumia stadi za maisha -Ni rahisi kijitumbukiza katika tabia mbaya za kujamiana -Kujiingiza katika tabia zisizo na maendeleo -Inaongeza matatizo ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana Baada a uwasilishaji wa masomo hayo VSI walipewa fursa ya kuuliza maswali kuhusiana na waliyofundishwa na maswali yote yalijibiwa na VSIi waliahidi kujafanyia kazi waiyofundishwa. Orodha ya Wawezeshaji Mafunzo haya yaliendeshwa na wawezeshaji wafuatao Upendo Person Gamalieli Mbalase John Kessy Orodha ya washiriki 1. Mwanahawa M Shayo 2. Mwajuma Bakari 3. Mariamu juma 4. Halima Hashimu 5. Zainabuu Hashimu 6. Magreth Robinson 7. Aviti Mustafa 8. Anjiti Mustafa 9. Niteshi Mustafa 10. Rashidi Issa. 11. Deo Frank 12. Japhet Yohana 13. Stivin Dobald 14. Merry stephano 15. Josephine JAMES 16. John Godfrey 17. Athumani Gabon 18. Mapinduzi Ally 19. Bakari hasani 20. Hamza Mudy 21. Lydia Joseph 22. Elizabeth Gasper 23. Amani Raphael 24. Swahumu Isa 25. Merry Stephano 26. Lillian Alex |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe