Fungua

/simbali/team: Kiswahili: WIqKljn9RnGqKpg07YSxEKLf:content

« Iliyotangulia   ·   Ifuatayo »
Asili (Kiingereza) Kiswahili

TARATIBU ZA CHUO

  1. Mwanachuo anatakiwa kuwa mfano mzuri wa nidhamu wakati wote awapo Chuoni.
  2. Mwanachuo anapaswa kuvaa “Uniform” pamoja na “Apron” au “Overcoat” awapo chuoni.
  3. Mwanachuo anapaswa kufika chuoni kwa wakati na kuondoka kwa wakati uliopangwa.
  4. Mwanachuo ahudhurie Chuoni siku zote za masomo na ashiriki kikamilifu katika mafunzo.
  5. Mwanachuo anapaswa kutoa dharura kwa mhusika kwa njia yoyte ile iwapo hatahudhuria chuoni au anapotaka kuondoka Chuoni kabla ya wakati uliowekwa.
  6. Mwanachuo ahakikishe analipa malipo yote ya mafunzo (Tuition fees) kwa utaratibu uliowekwa na Chuo.
  7. Mwanachuo atapaswa kulipia vifaa vya awali, ziara ya masomo, mitihani, mahafali na cheti kwa utaratibu uliowekwa na chuo.
  8. Iwapo mwanachuo atashindwa kulipa mafunzo kwa utaratibu uliowekwa bila ya sababu za msingi zinazoeleweka na uongozi anaweza kuzuiliwa masomo na hatimae kufukuzwa.
  9. Iwapo mwanachuo atakatisha masomo bila sababu ya msingi akiwa tayari amelipa gharama za masomo, basi hatarejeshewa malipo hayo.

10. Mwanachuo anapaswa kutunza vyema mazingira yote ya Chuo ikiwa ni pamoja na zana / vifaa vya Ofisini, Darasani, Jikoni, Chooni, “Workshop” n.k.

11. Iwapo mwanachuo atafanya uharibifu wowote ule wa mali ya chuo kwa kukusudia, atalazimika kulipa gharama zote za uharibifu huo.

12. Mwanachuo anayo fursa ya kutumia zana na vifaa mbali mbali vya Chuo kwa siku zote za wiki, ila tu amuombe mhusika.

13. Mwanachuo anayo fursa ya kukopa mashine ya kazi (charahani/overlock) kwa masharti yaliyowekwa na chuo.

14. Mwanachuo yeyote atakae kiuka taratibu hizi, hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.

 

KIAPO

Mimi ……………………………………………..……. naahidi kufuata taratibu zote zilizopo hapo juu.

 

…………………………………                             ………………………………..

Sahihi ya Mwanachuo                                            Sahihi ya Mdhamini/Mzazi

                                               

Sahihi ya Mkuu wa Chuo ……………………..

 

 

 

The Modern Tailoring Academy                                                       Tel 0777 – 465785 / 0777 - 849219Magomeni Zanzibar

 

(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe