Envaya

/tarucodefu/news: Kiswahili: WI000A60CB1DC7A000004298:content

Asili (Kiswahili) Kiswahili

Hivi sasa TARUCODEFU imekamilisha shughuli za utafiti shirikishi vitendo kuhusu tatizo la uhaba wa mai safi na salama kwa matumizi ya nyumbani linalo wakabili wakazi wa wilaya ya Mkuranga. Utafiti huu uligharimu jumla ya fedha kiasi cha shilingi za kitanania zipatazo 9,750,000/=. Fedha hizo zilipatikana kwa ufadhili wa shirika la utafiti na kupambana na umasikini nchini Tanzania la REPOA.

MAFANIKIO

Utekelezaji wa utafiti huu, umeleta mafanikio makubwa ambapo sasa jamii ya watu wanaoishi kando kando ya vijiji vinavyo zunguka vyanzo vya maji katika wilaya ya Mkuranga imetambua kiini cha tatizo lao na kwamba tayari umesha undwa mradi utakao saidia kuondosha tatizo hilo.

Hata hivyo utekelezaji wa mradi huu bado hauja anza kwa kuwa maombi ya fedha yaliyopelekwa kwa wafadhili bado hayajajibiwa. Tunaomba ushirikiano kwa wana Azaki wote ili kuweza kutekeleza mradi huo muhimu.

(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe