Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI WILAYA YA MULEBA- KAGERA
Shirika la Kwa wazee Nshamba Muleba kwa kushirikiana na Wazee ,walengwa liliadhimisha siku ya Wazee Duniani yaani tarehe 1 OTOBA 2012. Siku hiyo ilikuwa ya vifijo shangwe na nderemo kwa wazee wa kata saba za wilaya ya MULEBA na wanajamii waishio maeneo ya kata Nshamba, wajukuu wanao tunzwa na Wazee na wafanyakazi wa shirika, pamoja na wageni walioalikwa . Ikiwa ni mwaka wa nne kuadhimisha sherehe hizi , sherehe hiyo ilihudhuriwa na wazee wapatao 650 robo tatu yao wakiwa ni Wazee wanaopata pensheni toka shirika la Kwa Wazee. Michezo mbali mbali pamoja na nyimbo na risala vilivyoandaliwa na Wazee vilibeba ujumbe unaohusu maisha ya Wazee na changamoto wanozokumbana nazo, kama vile kutopatiwa matibabu bure, mzigo wa kulea na kutunza wajukuu, umaskini kwa wazee,na ukatili wanaofanyiwa Wazee lakini pia kuiomba serikali kutoa pensheni kwa wazee wote ili kuboresha maisha yao kama ambavyo nchi nyingine zimeweza kufanya. Akijibu risala hiyo, aliyekuwa mgeni rasmi katika madhimisho hayo Mhe Nashon Kababaye katibu tawala wilaya kwa niaba ya mkuu wa wilaya, Aliwapongeza wazee kwa kuona umuhimu wa kuadhimisha sherehe hiyo pia aliupongeza uongozi wa Kwa wazee kwa jitihada zao za kuboresha maisha ya wazee hapa wilayani Muleba. Mgeni rasmi alikemea vitendo vya ukatili kwa wazee na kuwataka waganga wote wanaopiga ramli kujisajiri kabla ya mwaka 2013 vinginevyo watakamatwa maana ndio wanaochangia vitendo hivyo. Pia mgeni rasmi alisisitiza na kutoa rai kwa wazee kuwa ni haki kwao kupatiwa matibabu bila malipo hivyo iwapo kutajitokeza utata alitoa namba za simu ili taarifa zitolewe ili uongozi uhusike kuwapatia ufumbuzi. Kuhusu pesheni kwa wazee wote alisema ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa upo uwezekano wa kulipa pensheni kwa wazee walio na umri wa miaka 60 na kuendelea. Aliomba ushirikiano na uwazi kwa matukio ya ukatili pindi yanapojitokeza ili kusaidia ufuatiliaji na kuwawajibisha wahusika. Aliwaomba wao pia, wawe na uchungu kwa maisha yao na mali zao. Naye kaimu mratibu wa shirika la kwa wazee , Ndg Edmund Revelian aliwapongeza na kuwashukuru wazee na wageni wote kwa mwitikio wao , katika maadhimisho hayo muhimu. Aliwaomba wanajamii na serikali kuuthamini uzee, kwani uzee si hiari bali ni hatua ambayo kila mmoja ataipitia.
|
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe