Base (Igiswayire) | Kinyarwanda |
---|---|
HAKI ZA WAZEE KWA MATAMKO YA SERA YA TAIFA YA WAZEE, MATAMKO YA KIMATAIFA NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAZEE
Haki ni stahili anayopaswa kupata mtu, kisheria ama kwa kuzaliwa, haki hiii humpa mtu uhuru wa kutenda au kumiliki (Chanzo:kanuni ya Oxford). Azimio la umoja wa mataifa namba 46 la mwaka 1991 limeweka bayana kuwa wazee wana haki zifuatazo:(i) kuwa huru (ii) kushiriki na kushirikishwa (iii) kutunzwa (iv) kujiendeleza/kukukza utu wake (v) kuheshimiwa [Chanzo: sera ya Taifa ya wazee 2003).
Kwa mujibu wa sera ya Taifa ya wazee, wazee wanakabiliwa na changamoto nyingi, kama umasikini, magonjwa, kutowekwa katika mipango ya maendeleo, n.k. Umasikini: Hii ni tatizo kubwa sana hasa kwa wazee wengi ambao walikuwa katika ajira zisizo katika mfumo rasmi kama wavuvi, wafugaji, wakulima wa mazao. Kwa sababu kundi hili halimo katika mfumo wowote rasmi wa hifadhi ya jamii. Pia wazee wastaafu walio katika mpango wa hifadhi ya jamii wanakumbwa na matatizo yanayotokana na urasimu wa kupata huduma (Chanzo: sera ya Taifa ya wazee, 2003). Mikakati iliyopo sasa haihusishi wazee katika kuondoa umasikini, hii ni kutokana kwa sababu hakuna sheria yeyote inayosimamia utekelezaji wa sera hii. Magonjwa:
Mipango ya maendeleo:
Kutokuwepo kwa mfuko wa wazee:
Kutokuwemo katika hifadhi ya jamii kwa wazee waliostaafu katika ajira zisizo rasmi:
MAPENDEKEZO: (i) Kutungwa kwa sheria: Kutokana na kutokuwepo kwa sheria yeyote inayosimamia utekelezwaji wa sera ya wazee, sera hii ya mwaka 2003 imebakia kuwa katika maandishi bila ,kuwepo katika vitendo. Hivyo basi kuwepo kwa sheria kutasaidia utekelezwaji wa sera. (ii) Halmashauri za wilaya zitenge fedha kupitia mfuko maalumu wa wilaya ili kuwawezesha wazee kupata huduma na pia kuendesha shughuli mbalimbali kupitia katika vikundi. (iii) Halmashauri kupitia idara ya maendeleo ya jamii na mipango iandae daftari la takwimu kubaini idadi ya wazee. (iv) Wazee kupata uwakilishi katika vyombo vya maamuzi katika ngazi zote za kata, Halmashauri na Bunge, hii itasaidia kuhakikisha kuwa hawasauliki kuwekwa katika mipango ya maendeleo, aidha kuhakikisha Bajeti inaweka fungu la kuwahudumia wazee. (v) Halmashauri kutengeneza mbinu/mfumo utakao wawezesha wazee kupata vyote Tiba na Dawa. (vi) Mgawanyo wa majukumu wa kuwasaidia wazee katika kutekeleza sera ya wazee uzingatiwe na kuwekwa katika vitendo kuanzia serikali kuu hadi ngazi ya familia. (vi) Baraza ya wazee yatimize wajibu wao wa kuhakikisha kwamba wanasimamia malengo ya uanzishwaji wa Mabaraza hayo ya kudai haki bora ya maisha ya wazee kwa ujumla.Hii ni katika ngazi zote kwa Mabaraza yaliyoundwa tayari, kwani ndiyo sehemu ya kupazi sauti za wazee. |
(Not translated) |
Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe