Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
@NABROHO SOCIETY FOR THE AGED (MAGU,MWANZA,TANZANIA): Wazee ni vijana wa zamani ambao walitumikia taifa hili katika nyanja mbalimbali za uzalishaji mali au katika kutoa huduma kwa jamii. Bila wao taifa hili lisingefika hapa lilipo leo na bila mchango wao tusingeweza kuwa na jeuri tuliyonayo leo au maendeleo tuliyofikia leo. Hivyo basi ni jukumu la vijana wa leo katika taifa hili kulinda mafanikio haya yaliyopatikana kutokana na wazee ambao ni vijana wa zamani. Ni haki kabisa kwamba wazee wanapaswa kulipwa bila kujali kama walikuwa waajiriwa wa serikali ama la. Nchi hii ina idadi ndogo sana ya watu walio katika ajira ya serikali au mashirika ya umma, lakini bado asilimia kubwa zaidi ya wazee wanalitoa mchango mkubwa katika taifa kwa kufanya shughuli zao binafsi, au katika kujiajiri wao wenyewe. Mchango huu usisahauliwe ama kutupwa eti kwa kuwa hawa watu ni wazee sasa. Wananastahili malipo kama shukurani kwa yale waliyoyafanya na ili kuwawezesha kuendelea na maisha yao na shughuli zao kabla Mwenyezi Mungu hajawachukua. |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe