Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
"Nawapongeza sana TEYODEN kwa kuwa na wazo la kubuni mradi huu kwa kuwa mwanzoni katika vikao vyao vya miradi iliyopita niliwasahuri kufanya mradi tangible(wenye matokeo ya kuonekana) haya ni matokeo ya kuufanyia kazi kwa vitendo ushauri niliyowapa."alisema bi Afisa vijana bi Anna Marrica "Mradi huu wa mama wadogo waliosahaurika utawawezesha wasichana husika kupata elimu,kujadili changamoto za maisha yao ya kila siku na baadae kupatiwa mitaji kwaajili ya miradi yao itakayoibuliwa katika vikundi.Mtumie mitaji kwa shughuli zilizokusudiwa na si vinginevyo."aliongeza bi Anna Marrica Wawezeshaji katika mafunzo haya walikuwa ni bwana Issa Tunduguru ambae ni Mkurugenzi wa Shirika la Poverty Fighting Tanzania na bwana Ally Manjasi ambae ni mkurugenzi wa Fedha wa shirika hilo. Katika mafunzo hayo pia tulipata wageni kutoka chuo kikuu cha Dar-es-salaam na mwanafunzi kutoka ujerumani ambae yupo Tanzania kujifunza kwa vitendo kazi za kijamii. |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe