Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
HALI HALISI YA MAISHA BAADA YA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM kama umebahatika kutembelea maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko katika jiji hili,hali ni mbaya sana kwa wakazi wa maeneo hayo.Nyumba nyingi ziko kwenye tope zito huku tope hilo likiwa limechanganyika na kinyesi cha binadamu. hali ya maisha kwa ujumla imekuwa ngumu sana kiasi kwamba wengine wamekata tamaa ya kuishi.Wapo wazazi ambao wana watoto wa shule,lakini tangu shule zinafunguliwa hawajaenda shule kutokana na kutokuwa na sare za shule na vifaa vingine vya shule. hili ni tatizo jingine ambalo linaweza kuwakumba wakazi wa maeneo haya ya bondeni.Ugonjwa wa kipindu pindu uko karibu sana kulipuka kama hatua za makusudi hazitachukuliwa.Chakula,maji,kulala,na hata kucheza kwa watoto ni katika mazingira machafu sana ambayo hayamfai mwanadamu aliye hai kuishi. nyumba za wakazi hawa wa bondeni,ukijaribu kuzitazama kwa umakini utadhani ni mabanda ya kuku au mbuzi,hakika inahuzunisha sana.Jamii yote ya kitanzania inalojukumu la kuwasaidia waathirika hawa ili kuhakikisha kuwa maisha yao yanazidi kusonga mbele kama ilivyo kuwa hapo mwanzo. katika maeneo haya misaada ya haraka inayohitajika ni kama vile nguo hususani kwa watoto wa shule,dawa kwa ajili ya kuulia mazalia ya mbu,vyandarua,dawa za kutibu maji,vifaa vya kufanyia usafi kama vile jembe,vyekeo,dastibini,na mifagio mikubwa. mitaro ya kupitisha maji machafu katika nyumba za wakazi hawa imeziba,hali ambayo inaongeza uwezekana wa kuleta maradhi zaidi katika maeneo hayo.Pamoja na tatizo lillilojitokeza,kuna umuhimu wa kutolewa kwa elimu ya mazingira kwa wakazi hao ili kuwakinga na maradhi yanayoweza kuwakabili muda wowote. zoezi la kuwasaidia waathirika wa mafuriko kuweza kuhama kutoka katika maeneo hayo linaonekana kwenda pole pole sana,hali ambayo inachangiwa na uwezo mdogo wa serikali kuwahudumia waathirika wote kwa pamoja.Kutokana na hali hiyo wito kwa mashirika ya kiraia,taasisi za dini na watu binafsi,washiriki kikamilifu katika kuhakikisha kuwa wanatoa misaada kwa wahanga hawa wa mafuriko. Kuendelea kufumbia macho watu wanao endelea kukaa bondeni ni kuwachimbia kaburi wakati wakiwa hai,hii ni kutokana na ukweli kuwa hata kabla ya mafuriko hali za wakazi hao ni mbaya sana kuanzia makazi na mazingira wanayoishi.Wito kwa wadau na watanzania wote wakazi wa bondeni ni ndugu zetu,tuwasaidie ili waweze kuondokana na hali waliyonayo kwa sasa.Waafrika tumezoea kusema 'kutoa ni moyo',usambe si utajiri.Saidia ili ibarikiwe.
|
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe