Base (Swahili) | English |
---|---|
WILAYA YA KONDOA NA VITUKO KATIKA ELIMU Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa iliyoko umbali wa kilometa 160 kutoka Dodoma inakabiliwa na hali mbaya ya maendeleo ya Elimu kufuatia shule zake za Sekondari kudorora katika matokeo ya mitihani ya kitaifa ukiwemo wa kidato cha nne uliofanyika mwishoni mwa 2010. Kufuatia matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyo tangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa mwanzoni mwa mwaka 2011; shule tano kati ya kumi zilizofanya vibaya kitaifa zilitoka katika Wilaya ya Kondoa ambazo ni Changaa, Kolo, Hurui, Kikore na Thawi. Hii ni hali halisi ilivyo katika chumba cha darasa kinachotumika kama ofisi ya walimu. Timu ya wanaharakati wa Elimu kutoka Asasi aya Marafiki wa Elimu Dodoma MED ilifanya ziara katika shule ya Changaa ambapo ilifanikiwa kufika kwa tabu kutokana na muiundombinu mibaya hasa ya barabara za kufika katika shule hiyo ambayo pia haina hata kibao cha kuelekeza jinsi ya kuifikia shule hiyo. Ziara ya Marafiki wa Elimu Dodoma ilibaini vituko vya aina yake katika shule hiyo yenye wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne na kuwaacha hoi kwa mshangao baada ya kubaini kuwa shule ya Changaa ina wanafunzi watatu (3) tu wa kidato cha nne kwa mwaka 2011 ambapo kati yao wasichana ni wawili na mvulana mmoja tu. Sababu za uwepo wa wanafunzi watatu wa kidato hicho ilielezwa ni kutokana na wengi wao kukata tamaa ya matokeo mabaya na pia umbali wa kutoka shuleni na makazi ya wenyeji. Wanafunzi wa shule hii tangu wajiunge na Elimu ya Sekondari hawajawahi kujifunza masomo ya Sayansi na Hisabati kutokana na kukosekana kwa mwalimu wa masomo hayo japo Mkuu wa shule hiyo ni walimu wa masomo hayo. Imeelezwa kuwa 2009 shule hiyo ilikuwa na mwalimu mmoja; 2010 walimu wawili na 2011 shule ina walimu watatu wa kuajiriwa na mmoja wa kujitolea na kulipwa posho na jamii. Wanafunzi wa Changaa wanatembea kwa zaidi ya kilomita sita kwa siku kwenda na kurudi shuleni kutokana na shule hiyo kuwa mbali na makazi ya watu jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa wengi wa wanafunzi hao kukosa hamu ya kuendelea na masomo. |
DISTRICT EDUCATION IN Kondoa and sights Kondoa District Council which is a distance of 160 kilometers from Dodoma facing a serious situation for the development of his school education following the secondary deterioration in the national examination results, including the Form Four was held at the end of 2010. Following the test results of which form four announced by the National Examination Council early in 2011, five out of ten schools for which came from the wrong national Kondoa District which is Changaa, Kolo, Hurui, garden and Thawi. This situation is in a class room, used as offices for teachers. A team of activists of Education from the Civil paragraphs Friends of Education Dodoma WITH conducted tour school Changaa which succeeded to the anarchy of muiundombinu bad, especially the roads to arrive at the school, which also does not even hit the guide on how to reach the school. Visit the Friends of Education Dodoma noted sights its kind in the school with students in forms one to four and left helpless by surprise after identifying that the school Changaa has students three (3) only in form four in 2011 when among them are two girls and one boy. The reason for the existence of three students is a form that was expressed by many of them despair of the poor performance and too far from local schools and homes. Students of this school since the join and Secondary Education have never learned the lessons of Science and Mathematics in the absence of a teacher of those subjects, though it is the principal teachers of these subjects. Indicated that in 2009 the school had one teacher, two teachers in 2010 and 2011 the school has three teachers employed by one of the volunteers and paid an allowance by the community. Changaa Students walk for more than six kilometers a day to and from school to school due to being away from home to something that has contributed significantly to many of these students lack the desire to continue with their studies. |
Translation History
|