Base (Swahili) | English |
---|---|
MED Yaomba Wastaafu Kufundisha kwa Mikataba.Asasi ya Marafiki wa Elimu Dodoma MED imemwomba Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushari ya Wilaya (DCC) Bw. John Tuppa; kuishauri kamati yake ili iwatumie walimu wastaafu kufundisha shule za sekondari za kata. Barua ya MED yenye maombi hayo iliwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya kwa lengo la kusaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu katika shule za kata katika Wilaya ya Dodoma. Kwa mujibu wa barua hiyo; MED imemuomba Bw. Tuppa kuwatumia walimu wastaafu kufundisha katika shule za kata ambazo wastaafu hao wanaishi badala ya kuendelea kuwasubiri vijana wadogo wanaohitimu masomo na kwenda kufundisha kwenye shule hizo bila kuzaa matunda tarajiwa. Barua hiyo ilieleza kuwa; licha ya nia ya serikali kuwatumia wahitimu wa kidato cha sita kuziba pengom la walimu; wahitimu hao wamekuwa wakituhumiwa kuwa sehemu ya chanzo cha ongezeko la mimba kwa wanafunzi wa shuleni wanazo fundisha. Baadhi ya wadau wameipongeza MED kwa hatua hiyo ya uthubutu waliyo ichukua kwa Mkuu wa Wilaya na kuongeza kuwa; wastaafu wengi wenye taaluma ya ualimu wana maadili ya kazi hiyo hivyo wanaweza kusaidia sana kupunguza tatizo la uhaba wa walimu kwenye shule za kata kama wastaafu hao watatumika ipasavyo na kupewa stahili zao. Mratibu wa MED Bw. Davis Makundi amekiri kumwandikia Mkuu wa Wilaya barua hiyo na kusema; hiyo ni haki ya msingi kwa mtu binafsi, taasisi au kikundi chochote cha kijamii kwani barua hiyo ni ya kumshauri na si ya amri kwa kiongozi huyo wa Wilaya.
|
WITH Teaching Contracts ask for pensioners.Institutions of the Community Education General imemwomba WITH Dodoma Dodoma Urban District, who also is chairman of the District Committee of evil (DCC) mr. John Tuppa, its committees to advise iwatumie retired teachers to teach secondary school in the county. WITH a letter of application that was presented to the District in order to help reduce the problem of shortage of teachers in county schools in the district of Dodoma. According to the letter, Mr. WITH imemuomba. Tuppa use retired teachers to teach in schools in the county where retirees live instead of continuous kuwasubiri young people who graduated and went to teach in these schools would bear the fruits expected. The letter stated that, despite the government's intention to use the Form Six graduates plug pengom of teachers, these graduates have been accused of being part of the source of conception increase of students at school they have taught. Some stakeholders have praised WITH the steps that the firmness which they took to the District and to add that, veterans most of the profession of teaching children the values of the work so they can help to reduce the problem of shortage of teachers in schools in the county as retirees they are used appropriately and given their deserved. Mr. WITH Coordinator. Davis has admitted Groups General District write a letter stating that: it is a basic right for an individual, institution or any social group, because this letter is to advise and not a command to the leader of the district. |
Translation History
|