Envaya

/Tawa/post/100107: Kiswahili: WI00035570F2BD7000100107:content

Asili (Kiswahili) Kiswahili

 

 

Survey ya Athari za Mafuriko,Keko Wilaya ya Temeke.

Yafuatayo ni Maswali na majibu:

1.Unaishi eneo gani

Mtaa wa Magulumbasi 'A'

2.Mtaa wako Unahitaji kitu gani sana sana

Mtaa wangu unahitaji

  • Kutengenezewa mirefereji midogo midogo itayoweza kuzunguka nyumba na kupitisha maji kwa urahisi sehemu zote.
  • Kutengeneza mipaka itayosaidia kutenganisha nyumba hadi nyumba.
  • Kuhamishwa na kutafutiwa maeneo ya kuishi.

3.Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba yako na vitu vyako

Vitu vyote vya ndani vilielea juu ya maji na kusombwa na kupotea,bidhaa zangu za biashara(Machinga) nazo pia zilipotea,(nguo za kike na za kiume,urembo)

4.Mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku

Baada ya kupoteza mtaji,maisha yameendelea kuwa mabaya maana hata pesa ya kula na kutunza watoto sina.

5.Vyanzo vya ubora wa maji kwenu vimepata athari gani kutokana na mafuriko.

Maji ya kutumia kwa matumizi ya kawaida ya kisima yamechanganyika na maji taka  hivyo kuleta athari za magonjwa ya mlipuko hasa kwa watoto.

6.Kama una kazi inachukua muda gani kutoka nyumbani kwako mpaka sehemu yako ya kazi.

Kwa sasa sina kazi baada ya mtaji wangu kupotea,ila wakati bado nna ajira ilikua inanichukua dakika 15 kufika sehemu yangu ya kazi.

 

 

 

(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe