Base (English) | English | |||
---|---|---|---|---|
WAGENI TOKA DAILY BREAD LIFE MINISTRIES KUTOKA IRINGA TAREHE 18/11/2019 Tarehe 18/11/2019 shirika letu lilitembelewa na ugeni kutoka Daily bread Life ministries kutoka Iringa. Kiongozi wa msafara alikuwa Askofu Mpeli Mwaisumbi wa kanisa la ACT FELLOSHIP ambaye ndiye mkurugenzi na mhasisi wa Ministri hii ya Daily Bread Life Ministries. Ugeni huu ulifika kwa lengo la kuweza kuona maendeleo ya shirika letu la FUTURE FOR TODAY PRIORITIES IN TANZANIA (FUTOPTA) kwa mwaka 2019. Waliweza pia kuongea na watoto wa shirika letu waishio katika mazingira magumu ilikujua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Aidha walifanya ibada ya pamoja na wanakijiji ambao walifika kwa kiasi kikubwa kuwasikiliaza na kujifunza mbambo mbalimbali. Hakika ilikuwa siku yenye furaha kubwa sana kwa wanakijiji wa Inolo na vijiji jirani. Pia walishiriki chakula cha pamoja pamoja na watoto na wanakijiji wote wa eneo ilo.
|
(Not translated) |