Asili (Kiswahili) | English |
---|---|
Wamiliki wa viwanda Tanzania waokoeni wakulima.
WAKATI wa uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Tanzania ilikuwa nchi ya Wakulima na Wafanyakazi. Katika kipindi hicho, wafanyakazi walikuwa ngangari hali kadhalika wakulima walikuwa wanaringa kutokana na kufaidi jasho lao. Ama kwa hakika wakazi wa Kilimanjaro, Mbeya na Kagera walikuwa wakulima wa ukweli wa kahawa, wakati wale wa Mtwara, Pwani na Lindi walijikita kwenye korosho. Kwa ujumla kila mahali wakulima walitekeleza wajibu wao. Sintawasahau wakulima wa mahindi wa Ismani huko Iringa wakishindana na wale wa Ruvuma na Rukwa wakati mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Mara wakulima wakijikita katika kilimo cha pamba huku Arusha hususan Mbulu ikiwa na ngano ama shayiri.. Kila mkoa kulikuwa na wakulima hodari i na Wafanyakazi walikuwa wakitekeleza majukumu yao kwenye ofisi, viwanda na mashirika mbalimbali ya umma bila uvivu. Tanzania ya enzi za Nyerere ilikuwa nchi yenye mipango iliyopangwa na kupangika, ingawa huruma ya sera ya ujamaa ambayo haikuweka sheria ya kumdhibiti kikamilifu anayeharibu mali ya umma. Udhaifu wa kutokuwapo kwa sheria ulisababisha viwanda, mashirika ya umma kutafunwa na wajamaa na kufa ‘kifo cha mende’. Pamoja na wafanyakazi kuendelea kuwapo, wakiwa katika vipande vipande chini ya Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (Tucta), Baada ya Nyerere kufariki dunia, mambo mengi yameharibiika, mfumo wa kilimo nchini. Wanunuzi wa mazao ya chakula hasa mahindi na mchele wanaonekana kwa vipindi wakitokea nchi za jirani, wakati wa mazao ya pamba, tumbaku, katani, na kahawa. Bila shaka Wazalendo wacha Mungu wenye viwanda vya kusaga unga wa mahindi ama ngano, kubangua korosho, viwanda vya kuchambua pamba na kusindika mafuta ya kula wana nafasi ya kusaidia kuboresha sekta ya kilimo. Wenye viwanda hivyo wanaweza kuwasaidia wakulima kama wataamua kununua mazao ya Watanzania badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi. Wamiliki wa viwanda hivyo wamekuwa wakinunua ngano, mahindi, shayiri, na mafuta ghafi ya kula kutoka nchi za nje zikiwamo Japani, Korea na China. Ni fedheha kwa wenye viwanda kuagiza mahindi nje ya nchi, wakati wanaweza kuwahamasisha na kuwahakikishia Watanzania walime mahindi mengi ili wayanunue.
|
Tanzania factory owners save farmers. During the leadership of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Tanzania was the Farmers and Workers. During this period, workers were likewise ngangari were small farmers to benefit from their labor. Indeed residents of Kilimanjaro, Mbeya and Kagera were coffee farmers truth, while those of Mtwara, Coast and Lindi were based on cashew. In general, farmers everywhere they perform their duties. Sintawasahau of Ismani maize farmers at Iringa contended with those of Ruvuma and Rukwa regions in Mwanza, Shinyanga and Mara farmers based on the cultivation of cotton with especially Arusha and Mbulu as wheat or barley .. Each region was strong in farmers and workers were performing their duties in the office, industrial and various public agencies without laziness. Era of Nyerere's Tanzania country program was planned and kupangika, though sympathy for socialist policies that are not fully ikuweka law to control who destroy public property. Weakness of absence caused by industrial law, public agencies eaten by socialists and die 'bugs' death'. With a staff continue to exist, in their pieces under the Federation of trade unions (TUCTA), After Nyerere died, many yameharibiika, farming system in the country. Buyers of food crops, especially maize and rice are seen intermittently coming from neighboring countries, while the crops of cotton, tobacco, and coffee. Of course the pious nationalists mills corn or wheat, crashing cashew nuts, cotton processing factories and processed edible oils have the opportunity to help improve the agricultural sector. Manufacturers so they can help farmers as they decide to buy products Tanzanians rather than importing from abroad. Owners of factories have been buying wheat, corn, oats, and eat crude oil from foreign countries zikiwamo Japan, Korea and China. It is a shame for the industry to import maize abroad, when they can motivate and assure Tanzanians that wayanunue Lime maize. |
Historia ya tafsiri
|