Hasante sana kwa mada yako na kutoa fursa katika kuchangia mada hii ya Wazee ni kweli unavyosema sisi vijana wa sasa ni tofauti kabisa na vijana wazamani ambao sasa ni wazee kumekuwa na vitendo vya unyanyasaji,ubaguzi kwa wazee utafikiri hawa wazee hakuwa vijana au sisi vijana hatutazeeka .
mimi japo ni kijana lakini nimepata mchango mkubwa sana kwa wazee mpaka nimefika hapa nilipo, ninasema wazee wanamchango mkubwa na wanafanya kazi kubwa kwa sababu wazee wanamaono ambao kama ingekuwa ni kulipia basi ungelipia kwa pesa nyingi sana na hata kama ungekuwa na hizo pesa wenda ungekosa maono hayo
ukiangalia vijana wengi kutokana kuadaiwa na ujana wanajikuta wanakuwa na watoto ambao mzigo huo wa watoto uwapelekea wazee .
si hivyo kijana anapopata matatizo hasa ya magonjwa makubwa na kutengwa na ndugu na malafiki ukimbilia kujiuguza kwa wazee ila wazee hawa mchango wao haujilikana ndani ya jamii na malipo yao uishia katika kusimagwa na kutengwa
wazee katika kulitumikia taifa ndio walikuwa kipaumbe katika kufanya matambiko ya kijadi lakini pia tunawategemea katika kujua historia ya miji,vijiji na mambo mbalimbali bila ya gharama yoyote
mwisho napenda kuishia kwa kusema wazee si kwamba wanaweza kufanya kazi ndogogo la wanafanya kazi kubwa sana kiasi kwamba hatuna mshahara wa kuwalipa