Sakale Development Foundation ni shirika lisilokuwa la kiserikali ambalo lilianzishwa mwaka 2006 na kusajiliwa rasmi na serikali tarehe 05/03/2007 kwa hati ya usajili namba OONGO/1258.
shirika lilianzishwa na wanachama waanzilishi 13 hadiĀ wakati huu shirika lina wanachama 21. Mipaka ya shughuli za shirika kwa mujibu wa usajili wake ni Tanzania bara hata hivyo kwa sasa shirika bado halija pata uwezo wa kushughulika katika eneo pana, hii ina maananisha kuwa kwa wakati huu tumejizatiti zaidi kufanya kazi katika eneo la wilaya ya Muheza na maeneo ya jirani, tutaongeza maeneo ya shughuli kwa kadri ya ongezeko la uwezo wetu.