Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Mafanikio ya POFADEO

Jumuiya hii tangu ilipoanzishwa imefanya mambo mengi. Jumuiya imewahi kushiriki katika maonyesho mbali mbali yayoandaliwa na The Foundation For Civil Socity ikiwa ni pamoja na yale maonyesho  yanayofanyika katika ukumbi wa baraza la wawakilishi Zanzibar, viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dodoma na viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam.

Katika maonyesho hayo, POFADEO inapata fursa ya kujifuza mambo mbali mbali kutokana na kuangalia shughuli za jumuiya nyengine ambazo pengine zinakuwa na uzoefu zaidi kuliko POFADEO, na vile vile POFADEO inapata fursa ya kuonysha shughuli mbali mbali zinazofanywa na jumuiya hiyo.

Miongoni mwa ajenda ambayo POFADEO imewahi kuwasilsha katika maonyesho Bungeni na Baraza la Wawakilishi likaleta msisimko mkubwa kwa waheshimiwa wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni utetezi wa haki za wanyama. Ajenda hii ilileta hoja kubwa kwa vile ilionekana ni ajenda ambayo ilihitaji kutiliwa maanani sana kutokana na umuhimu wa ajenda yenyewe hasa ukitilia maanani kuwa ukatili dhidi ya wanyama umepamba moto hususan katika kisiwa cha Zanzibar. Miongoni mwa vitendo vya kikatili ambavyo vinafanywa dhidi ya wanyama hapa Zanzibar ni pamoja na kubebeshwa mizigo mizito kinyume na uwezo wa wanyama hao, kupigwa viboko kiholela, na wakati mwengine kufanyishwa kazi wakiwa wanaumwa au wakiwana njaa.

Ajenda hii iliata hoja nyingi kutoka kwa wajumbe mbali mbali walioshiriki katika maonyesho hayo, lakini cha msingi kila mmoja alikubali kuwa wanyama wananyanyaswa na hivyo jamii inapaswa kuzingatia umuhimu wa kuchunga haki za wanyama kama viumbe wengine.

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kutambua umuhimu wa haki za wanyama, ilipitisha sheria ya wanyama ya mwaka 1999 inayojulikana kwa jina la "Animal Resources Management Act 1999".

Jambo la kusikitisha ni kwamba sheria hiyo imebaki tu katika vitabu lakini jamii ya wa Zanzibari wengi hawaijui. POFADEO kwa upande wake inajaribu kuielimisha sheria hiyo kwa jamii lakini inahitaji kupata msukumo wa ufadhili ili iweze kuwafikia wanajamii wengi zaidi.