Envaya
Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

Pemba Basketball Club yapokea mipira 40 kutoka Ubalozi wa Marekani Tanzania.

Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani, J. Michael Tritchler, akimkabidhi mipira mgeni rasmi kutoka Afisi ya Mkuu wa Wilaya Mkoani - Pemba, Afan Othman Juma. Kulia ni Raisi wa Pemba Basketball Club, Hussein Matora Hussein.

 

Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani, J. Michael Tritchler, amekabidhi jumla ya mipira 40 ya basketball kwa Pemba Basketball Club kwa niaba ya Balozi wa Marekani nchini Tanzania. Amesema katika hafla ya upokeaji wa msaada huo katika ukumbi wa Umoja ni nguvu Mkoani, Pemba kwamba nchi yake itaendelea kusaidia Pemba Basketball Club kila itakapowezakana.

Naye Mgeni rasmi katika hafla hiyo, ndugu Afan Othman Juma kwa niaba ya afisa tawala Wilaya Mkoani – Pemba, amesifu jitihada za viongozi wa Pemba Basketball Club na pia ametoa shukrani kwa Ubalozi wa Marekani. Katika kuendeleza mbele klabu hiyo amehidi kuchangia fedha taslimu 50,000/=.

Raisi wa Pemba Basketball Club, Hussein Matora Hussein, ametoa shukrani za dhati kwa Ubalozi wa Marekani na watu wa Marekani kwa msaadu huo. Amesema klabu ipo pamoja na watu wa Marekani na inaahidi kutoa masharikiano makubwa kwa watu wa Marekani. Pia Raisi alisisitiza suala la elimu na amesema kwamba mbali na kutoa mafunzo ya mchezo huu, klabu pia inatoa stadi za maisha kwa vijana kwa lengo la kuepusha na janga la madawa ya kulevya na vikundi viovu. Raisi ametoa wito kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi kuiga mfano wa nchi ya Marekani katika kusaida klabu hiyo.

Ubalozi wa Marekani mbali ya msaada huo wa mipira, imewahi kumpeleka raisi wa Pemba Basketball Club nchini Marekani kwa mafunzo ya mpira huo katika mwaka 2010.

Pemba Basketball Club imeanzishwa mwaka 2011 na imepata usajili rasmi kutoka Wizara ya Michezo Zanzibar terehe 10/1/2012. Kwa sasa klabu ina vijana 63 wenye umri chini ya miaka 14, ina jumla ya wakufunzi wanne tu.

 

19 Juni, 2012
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.