Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Kwanini watanzania tulio wengi ni masikini hata wa mawazo.

Godlisten Msaki (nyengedi)
May 6, 2012 at 10:00 PM EAT

sihitaji hadithi za rasilimali tulizo nazo, zinaboa tunazijua

Wadau karibuni

 

Venitha Bishanga (UDOM)
May 7, 2012 at 12:51 AM EAT

@Godlisten Msaki (nyengedi): 

Venitha Bishanga (UDOM)
May 7, 2012 at 12:56 AM EAT
Ni kwa sababu hatujiamini.
fikiri mvugaro (mwela vuga)
May 11, 2012 at 10:29 AM EAT

watanzania tulio wengi ni mabigwa na wataalamu wazuri wa mawazo hasa wanasiasa wetu ila tatizo linapokuja pale inapofikia utekelezaji ndio mbinde ukitaka kuamini hilo angali kipindi cha uchaguzi kinapofia uambiwa maneno matamu na yakutia moya hata kama ulikuwa huna haja ya kupiga kura utahamasika mwenyewe kwenda kupiga kura. si hivyo tu kama mfuatiliaji mzuri kipindi cha majadiliano au utoaji wa muswada bungeni mawazo yanatoka mazuri na yakutia moyo ila sasa inapokuja kwenye utekelezaji

nazidi kuamasika kukutolea mifano wa Sera na mikakati mingi ya serikali kama umebaatika kuiyona utaona mawazo na maono mazuri yaliyojaa katika sera hizo na mikakati hiyo. hayo yote ni mawazo ya watanzia yaliyo mazuri swali la kujiuliza ni kwanini mawazo hayo hayatekelezeki?

Albert (Arusha)
June 5, 2012 at 9:44 AM EAT

Nakumbuka siku moja aliyekuwa Raisi wa Msumbiji wakati akiaga Watanzania...kipindi cha Mzee Mkapa alipokuwa akijibu hotuba ya Mkapa(ya Kiingereza) yeye alijibu kwa Kiswahili sanifu alisema huku akicheka."Maendeleo tunayoyafanya Msumbiji tumeiga sera na mipango yote ya Tanzania wakati tukiwa Nachingwea. Sisi Msumbiji ndio tunapaswa kujifunza zaidi kutoka Tanzania". Kwangu  mimi nilijisikia aibu sana kama Mtanzania.

Sisi Watanzania kinachotumaliza ni ubinafsi wetu hasa Viongozi.Kila mtu anataka kuwa Bill Gate.....kwa pesa ya KODI. Hakuna miradi mipya ya uzalishaji, tekinolojia mpya kila mmoja anataka kutembelea (Hummer, Vog)


Add New Message

Invite people to participate