Mapambano dhidi ya umasikini na UKIMWI Ni shirika lisilo la kiserikali lililo anzishwa tangu mwaka 2006 na watu wachache waishio na VVU / UKIMWI wazo la kuanzisha asasi hii lilikuja baada ya kutafakari changamoto mbalambali zinazowakabili watu waishio na vvu /ukimwi ktk maisha yao kwa ujumla Hii ilipelekea kuanzishwa kwa mradi wa bustani ya mbogamboga ili kujipatia mbogamboga kwa ajili ya lishe lakini pia wanachama wameweza kuanzisha mradi wa ufugaji wa mbuzi wa asili wa nyama na maziwa kazi hizi zote zinaendana sambamba na utoaji wa elimu ya ukimwi kwa jamii mikutano ya hadharo COMMUNITY EVENT kupitia vyombo vya habari na television maduu ina ofisi yake magomeni kagera kata ya ufukoni ingawa ilianza na watu sita kwa sasa ina wanachama ishirini na tano na imesajiliwa tarehe 16 november 2010 act no 24 ya 2002 wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto
18 Mei, 2011
Maoni (2)