Envaya

UTANGULIZI

Asasi ya Mapambano Dhidi ya Umasikini na Ukimwi ni Asasi isiyo ya kiselikari na isiyolenga kugawana  faida lakini inalenga kutoa ushauri wa kuendesha miradi ya kiuchumi kwa waathirika na waathiriwa wa janga la UKIMWI.  Asasi hii imeanzishwa na watu wachache wanaoishi na virusi vya UKIMWI  Tangu mwaka 2006

Asasi hii imeundwa Baada ya kutafakari kwa kina  matatizo  mbalimbali yanayotupata wa tu tulioathirika na VVU/UKIMWI Yanahitaji nguvu ya pamoja ili tuwe na maendeleo ya afya zetu

ikiambatana na huduma mbalimbali za kijamii.

DIRA YA ASASI

Kuwa na jamii yenye maendeleo na ustawi kwa ujumla bila kujali tofauti za kijinsia kuboresha mazingira na kutokomeza umasikini ifikapo mwaka 2025

DHAMIRA YA SHIRIKA

Kupunguza athari za kiuchumi na kijamii, kuwezesha kwa mafunzo na ushauri wa kuendesha miradi ya kiuchumi kwa waathirika na waathiriwa wa VVU/UKIMWI ili kuwa na jamii yenye afya bora na uendelevu wa huduma mbalimbali kwa ujumla na kuimarisha ushirikiano.

 

MADHUMUNU

Kupunguza athari za kiuchumi na kijamii zitokanazo na hali ya kuathirika na kuathiriwa na VVU/UKIMWI Ktk mkoa  wa Mtwara.