Envaya

Hakuna Maisha Bora Bali Bora Maisha.

Familia moja katika Kata ya Kikuyu Kusini Manispaa ya Dodoma itaubaliana na kauli yangu kwa Bora Maisha kwa Kila Mtanzania na ukweli si Maisha Bora kwa kila Mtanzania kama ambavyo kauli hiyo imekuwa ikiimbwa kila kukicha na viongozi wetu wa Serikali na hata wa hama Tawala CCM.

Kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu sasa moja kati ya nyumba zilizoathiriwa na mvua zilizonyesha mjini Dodoma tangu mwishoni mwa mwezi Januari haijafanyiwa ukarabati licha yafamilia hiyo kuendelea kuitumia nyumba hiyo huku kila siku wakizidisha sala na kujikabidhi mikononi mwa muumba kwa lolote linaloweza kutokea.

Unadhani familia hii itachagua lipi kati ya  Maisha Bora kwa Kila Mtanzania na Bora Maisha kwa Kila Mtanzania? Ni wazi kwamba jibu la familia hii unalo. Tuachane na nyumba ya mpiga kura huyu na kuangalia suala la usafi wa mazingira na hasa suala la choo; KARIBU!

Hiki ndicho choo kinacho tumiwa na familia hii; hiki ni kipindi cha mvua ambacho kwa kawaida kipindupindu nacho hushika hatamu. Bado najiuliza juu ya Familia hii; inaihesabu na kuikubali SERIKALI NA KAULI ZAKE? Majibu na ushauri wako ni muimu sana!

16 Machi, 2011
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.