MED YATOA SAADA WA VITABU.
Shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma MED limetoa msaada wa vitabu vya kiada na kiongozi cha mwalimu vyenye thamani ya zaidi ya Sh. 397,363,300 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa lengo la kuboresha Elimu katika Wilaya hiyo. Mdsaada huo wa vitabu vya masomo ya kiingereza, Hisabati na Jiografia utawanufaisha walimu na wanafunzi wa shule 82 za Halmashauri ya Chamwino iliyoko Mkoani Dodoma.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Handali ambayo ni moja kati ya shule zilizonufaika na msaada huo wa vitatu mwalimu Grace Mtani alisema msaada huo umekuja atika wakati muafaka hasa ukizingatia kuwa utakuwa ni msaada mkubwa hasa kwa wanafunzi wa darasa la saba ambao wapo kwenye maandalizi ya mtihani wa taifa. Akionyesha kuwa nia yao ni kutaka kusaidia jamii inayowazunguka kwa wakati mratibu wa shirika hilo la marafiki wa elimu mkoani Dodoma Bw. Davis Makundi amesema msaada huu ni mwanzo tu katika halmashauri hiyo ya Chamwino,kwani wamejipanga vizuri kwa kushirikiana na wadau wengine katika kuboresha elimu ya wanaChamwino.
Mbali na msaada huo wa vitabu katika wilaya hiyo, MED imeweza pia kushuhudia matatizo mengi yanayowakabiri wanafunzi wengi katika wilaya hiyo hasa likiwemo tatizo la ukosefu wa madawati kitu ambacho kimeonekana kama kuwa ni tatizo lililoanza kuzoeleka katika maeneo mengi katika wilaya hiyo, pia limejtokeza tatizo kubwa linalohatarisha afya za wanafunzi wengi katika shule nyingi katika wiaya ya chamwino ni ukosefu wa vyoo, vyumba vya madarasa, madawati, zana balimbali za lujifunzia na kufundishia pamoja na mafunzo ya walimu kazini.
Comments (1)