Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

MED KUGHARAMIA MITIHANI YA MAZOEZI IV KIKUYU SEKONDARI.

Shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma MED litagharamia uchapishaji wa mitihani ya Mazoezi kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Kikuyu ili kuongeza maarifa kwa wanafunzi wa shule hiyo wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwezi Novemba, 2013.

Uamuzi huo wa MED umetolewa katika kikao cha pamoja kati ya wazazi, wanafunzi na walimu wa kidato cha nne wa shule hiyo kilichoitishwa kwa lengo la kutathimini matokeo ya kidato cha Nne 2012 na kujipanga kwa ajili ya matokeo ya mtihani wa mwaka huu.

Akichangia katika kikao hicho Mratibu wa MED Bw.Davis Makundi Amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa wahitimu wa mwaka huu wanafanya vizuri  hapana budi jamii,walimu,wazazi,wanafunzi na wadau mbalimbali kuungana pamoja kuwawezesha wanafunzi kupata mazoezi ya mara kwa mara ya majaribio ya mitihani ya kujipima

Akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne 2013 kwa wazazi mwalimu wa taaluma shuleni hapo Francis Tumaini  Wambura amesema kidato cha nne kwa mwaka huu kina wanafunzi 168 ambao wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne.

Kwa mujibu wa taarifa za idara ya taaluma shuleni hapo kati ya  wanafunzi 168 wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu wanafunzi 21 mpaka sasa hawaja sajiliwa kutokana na utoro.

Aidha taarifa zimeongeza kuwa  zoezi la kulipia ada ya mtihani wa taifa linalotarajia kukamilika tarehe 28 mwezi huu wa pili inaonekana kusuasua ambapo wanafunzi 40 pekee ndio waliolipia ada hiyo hadi sasa.

February 23, 2013
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.