Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

NDEBWE YALETA MABADILIKO KATIKA DEMOKRASIA.

Na. MED Information Unit

Shule ya Msingi Ndebwe iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma imeonesha matokeo mazuri katika uchaguzi wa kidemokrasia kwa kumchagua msichana kuwa Kiranja Mkuu wa shule hiyo na kuwashinda wavulana waliokuwa wapinzani wake wa karibu.

Rosemary Masaka (pichani) mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Ndebwe alipata ushindi huo baada ya kuamua kugombea nafasi ya kiranja Mkuu kufuatia mafunzo ya elimu ya kidemokrasia katika kuwapata viongozi wa shule yaliyotolewa na shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma (MED) kupitia mradi wake wa Haki zangu Sauti Yangu unaofadhiliwa na shirika la Oxfam GB.

Akiongea na maafisa wa MED mtoa habari hizi ambaye hakutaka jina lake litajwe alieleza kuwa hii ni mara ya kwanza shule yao kupata kiranja Mkuu mwanamke. “zamani tulikuwa tuna chagua viongozi sisiwenyewe walimu na kuwatangazia wanafunzi” alisema mtoa habari huyo.

Aliongeza kuwa awali shule ilikuwa zikichagua viongozi kwa cheo cha kaka Mkuu na Dada Mkuu ambapo sasa utaratibu umebadilika na kuwapata viongozi hao kwa cheo kipya cha kiranja Mkuu bila kujali jinsia.

Mradi wa My Rights My Voice ni mradi wa miaka mitatu (2012 – 2014) unaotekelezwa katika shule 16 za msingi na 4 za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa lengo la kuimarisha ari ya watoto kujifunza na kuanzisha mabaraza ya wanafunzi kwa kuendesha chaguzi za kidemokrasia katika kuwapata viongozi wake.

February 18, 2013
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.