Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Ben Pol aonesha kuwa msanii ni kioo cha jamii


Ben+pol.jpg
Ben Pol msanii wa bongo flavor na mshindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro 
kwa mwaka 2011 na 2012 akiwa na bango la 'Boresha Chekchea'.

 Ule usemi wa kuwa msanii ni kioo cha jamii unajidhirisha kwa msanii wa mziki wa bongo flavor Bernard Michael Paul Mnyang'angaanae julikana kisanii kama Ben Pol kuunga mkono kampeni ya kuboresha elimu ya awali Tanzania.

Kampeni hiyo ilizinduliwa na HakiElimu tar 27 September 2012 iliyoambatana na uzinduzi wa matangazo mawili ya Television na redio kwaajili ya kuendeleza kampeni hii ya elimu ya awali iliyopewa jina la Chekechea.Matangazo hayo yanaonesha changamoto zilizoko katika elimu ya awali nchini na kutoa mfano wa shule bora au elimu ya awali inayotakiwa nchini Tanzania
 
BEN.jpg
Ben Pol akiwa katika baadhi ya kazi zake za kisanii jukwaani

 
Elimu ya Awali ni muhimu kwa maendeleo ya mtoto kimwili, kiakili na kimaadili. Katika Sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 1995 Serikali inaonesha umuhimu wa elimu ya awali,inapotamka ; “Tafiti kadhaa zilizofanyika nchini katika miaka ya 1980 zilibaini kuwa watoto waliopitia elimu ya awali huwa na mafanikio makubwa zaidi wanapoanza darasa la kwanza. Kutokana na kutambua umuhimu huu, Serikali iliamua kuingiza Elimu ya Awali kwa watoto wenye umri wa miaka 5 na 6 kwenye mfumo rasmi wa elimu na kila shule ya msingi inapaswa kuwa na madarasa ya Elimu ya Awali.”
Sera ya Elimu na Mafunzo 2010. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi . Toleo jipya Rasimu ya 2 March 2011.(uk 5-6).

Uwekezaji katika huduma bora kwa mtoto na elimu ya awali huwa na faida maradufu kwa watoto wetu- ambao ni raia wetu wa  baadaye. Walipa kodi nao pia hufaidika na huimarisha uchumi. Faida ya uwekezaji wa fedha za umma katika elimu bora ya awali ni kubwa sana. Lakini je, Tanzania imeligundua hili na kulitekelezakikamilifu?  Na je, maneno haya ambayo sera inasisitiza yako yanatekelezwa kwa vitendo?

Baada ya kufanya tafiti katika sehemu mbalimbali nchini  HakiElimu inasikitishwa na jinsi ambavyo elimu ya awali inavyotolewa katika mazingira yasiyofaa hali inayochangia kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.  Kama ilivyo katika elimu ya msingi na ile ya sekondari , elimu ya awali imegubikwa na changamoto nyingi. Baadhi ya changamoto hizi ni  upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, unaosababisha mrundikano mkubwa katika madarasa,  ukosefu mkubwa wa walimu wenye taaluma ya elimu ya awali pamoja na vifaa vya kufundishia. Aidha, kutokuwepo na tofauti ya kimadarasa katika elimu ya awali ( yaani watoto wa umri wa miaka 5 na miaka 6 kusoma katika darasa moja), na wingi wa masomo pia ni changamoto.

Haki Elimu HakiElimu

@misstamarind Tutafurahi kama utatufafanulia ujumbe huu una maana gani umetuacha mbali sana

Haki Elimu HakiElimu

Mwanafunzi wa shule ya sekondari Bukoba azuiwa kufanya mtihani wa #kidatochaIV kutokana na kuwa na ujauzito - Mwananchi pg3

Haki Elimu HakiElimu

Tuzo za wandishi bora wa mwaka 2012 zimezinduliwa rasmi leo na wadau wa MCT. Elimu ni mojawapo kati ya 18 maeneo... http://t.co/mIDG3M8P

Haki Elimu HakiElimu

@ludadaud Fuatilia TL ya @njamason kufahamu sababu kubwa inayowasababisha kuzuiliwa kufanya mitihani, tena kigoma tuliwahi kuripoti hilo

Haki Elimu HakiElimu

@Allan_Lucky "Rais wa Wanafunzi" tufikishie hii http://t.co/EMjE57Kq kwa wananchi wako michango yao tunaisubira hapa http://t.co/pdebCzsx

Haki Elimu HakiElimu

@ludadaud Vipi tena tujuze yaliyojiri na huko usisahau TT ni #kidatochaIV

Haki Elimu HakiElimu

Mwanafunzi afanya mtihani #kidatochaIV akiwa wodini baada ya kufanyiwa upasuaji, asema hayuko tayari kuikosa mitihani hiyo- Mwananchi

Haki Elimu HakiElimu

Wanafunzi 97 huko Kahama kutokufanya mtihani wa #kidatochaIV kutokana na kukosa fomu za maendeleo akiwa shule ya msingi (TMS9)- Nipashe