Mbali na tovuti ya Envaya, baadhi ya mashirika tayari wana tovuti, blogu, au Facebook au Twitter.
Envaya inakuwezesha kuunganisha tovuti yako ya envaya na tovuti nyingine za asasi yako. Hii inaruhusu watu wanaoangalia tovuti yako ya Envaya kutembelea tovuti zako mengine.
Kuongeza tovuti nyingine kwenye tovuti yako ya Envaya, nenda kwenye ukurasa wa hariri Tovuti ( ), Na hariri ukurasa mkuu. Kisha, bonyeza tovuti nyingine Ingiza anwani ya tovuti ambayo kitajenga kiungo kwenye ukurasa wako wa Envaya.
Wakati wa kuhariri ukurasa wowote wa Envaya, unaweza bonyeza ili kujenga kiungo, kisha ingiza anwani ya ukurasa unaotaka kuunganisha.
Kuagiza Ukurasa Kutoka Blog, Facebook, au Twitter
Kama asasi yako tayari ina blog, akaunti ya Facebook au Twitter , unaweza kuingiza moja kwa moja kwenye ukurasa wa Habari wa tovuti yako ya Envaya.
Nenda kwenye ukurasa Hariri Ukurasa ( ), aa hariri ukurasa mkuu. Kisha, nenda chini kwenye Habari kutoka tovuti nyingine. Ingiza anwani ya tovuti yako nyingine na ujenge kiungo kwenye ukurasa mkuu wa Envaya.
Kila ukibadilisha kitu chochote kwenye tovuti yako itaonekana moja kwa moja kwenye ukurasa wa Habari katika tovuti yako ya Envaya baada ya dakika chache.