Envaya

Envaya

Kuhariri Kurasa kwenye Tovuti yako

Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka Kiingereza, lakini tamko la Kiswahili ni la zamani. Ona asili · Hariri tafsiri
Msaada : Kuhariri Tovuti Yako

Kuhariri Kurasa kwenye Tovuti yako

Katika ukurasa wa Hariri Tovuti ( ) ipo sehemu ya Hariri Kurasa, ambayo inaorodhesha kurasa zote za tovuti ya shirika lako. Hapa unaweza kuhariri ukurasa uliopo, kubadili utaratibu ya kurasa, au kuongeza ukurasa mpya kwenye tovuti yako.

Kurasa zilizopo katika tovuti yako zinaorodheshwa kwa kutumia "bold", juu ya mstari kijivu, katika utaratibu kama zinazoonekana katika menyu ya tovuti yako. Ili kuhariri ukurasa, bonyeza jina lake.

Upande wa kulia, kuna "mishale ya juu" ambayo inakuruhusu kubadili utaratibu wa kurasa katika menyu ya tovuti yako. Kwa kubonyeza mshale, unaweza kusogeza ukurasa sambamba kuelekea mwanzo wa menyu ya tovuti yako. Ukurasa uliopo juu ya orodha unatumika kama ukurasa wa mwanzo wa tovuti yako.

Kutegemea ukihariri ukurasa gani, hatua mbalimbali zitatakiwa ili kuhariri ukurasa fulani. Hata hivyo, kurasa nyingi, kama vile Historia, Miradi, na Timu, zina boksi kubwa nyeupe, inayoonekana kama hii:

Katika boksi hii, unaweza kuandika maandiko na kuingiza picha au hati. Unaweza pia "copy-and-paste" maandiko kutoka maeneo mengine, kama vile hati za Microsoft Word.

: Kuumba kiungo na tovuti nyingine, ama kwenye tovuti yako au mahali pengine.
: Kuingiza picha 
: Kuingiza faili nzima ya hati, kama vile Microsoft Word, PowerPoint, PDF, n.k. 
: Kuhifadhi mabadiliko yako (bila kuyachapisha), ili usipoteze  kazi yako.
: Kurudisha ukurasa wako kwa toleo la awali.

Kuongeza Kurasa Mpya

Katika ukurasa wa Hariri Tovuti ( ), chini ya sehemu ya Hariri Kurasa kuna orodha ya kurasa zinazopendekezwa uziongeze kwenye tovuti ya asasi yako, na pia kiungo cha Ongeza ukurasa mwingine, ambacho kinakuruhusu kuongeza ukurasa wowote unaotaka.

Wakati unapobonyeza Ongeza ukurasa mwingine, hatua inayofuata ni kuchagua jina la ukurasa litaloonyeshwa katika menyu ya tovuti yako, na kisha kuongeza maandiko (na picha) kwa ukurasa wako mpya. Mwishoni, bonyeza kitufe cha Umba ukurasa ili kuchapisha ukurasa wako mpya katika tovuti yako.

Njia nyingine kwa Kuhariri Kurasa

Wakati ambapo umefungua Envaya, na unapoangalia tovuti yako, unaweza kubonyeza Hariri Ukurasa katika juu-kulia ili kuhariri ukurasa wa sasa, kama hapo chini:

Kufuta Kurasa

Kama ukitaka kuondoa ukurasa kutoka tovuti yako, kwanza, fuata hatua hapo juu ili kuhariri ukurasa. Kisha, bonyeza kitufe chekundu cha Futa ukurasa, kama hapo chini:

Iliyotangulia: Kuandika Habari