Envaya

Envaya

Kuchagua Usanii wa Tovuti yako

Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka Kiingereza kwa Kiswahili. Ona asili · Hariri tafsiri
Msaada : Kuhariri Tovuti Yako

Kuchagua Usanii wa Tovuti yako

Wakati umeingia kwenye akaunti yako ya Envaya, unaweza kubadlisiha muonekano wa kurasa wa tovuti ya shirika lako, kama vile nembo au kichwa itakayoonekana juu ya kila ukurasa, na kuchagua mandhari (picha au rangi) kwa ajili yako tovuti.

Kutoka ukurasa wa kuhariri tovuti   , Nenda

kwenye sehemu ya Links na bonyeza Hariri usani wa tovuti, kama inavyoonekana hapo juu.

Kuongeza Nembo ya Shirika lako

Nembo ya asasi yako ni picha ndogo ambayo inaonekana karibu na jina la asasi yako juu ya tovuti yako ya Envaya, na katika maeneo mengine mengi juu ya Envaya.

Unapojiandikisha Envaya, nembo ya shirika lako ni ramani ndogo ya mji ambapo shirika lako lipo.

Kubadili nembo hii, nenda kwenye sehemu ya Organization logo kwenye ukurasa wa Hariri usanii wa tovuti, karibu na "picha Mpya" (inaweza kusema Browse, lakini inategemea na kompyuta yako).

Kisha, chagua picha ya nembo ya asasi yako kwenye kompyuta yako.

Kama Envaya inaweza kuelewa faili uliyoichagua, itaonyesha hakikisho nembo yako, kama hapa chini. Bonyeza kitufe cha bluu kuhifadhi mabadiliko ya nembo yako. 

Kama kuna matatizo kwenye kuweka nembo yako, unaweza kutuma nembo yako kama faili kwa njia ya barua pepe kwa kutumia admin@envaya.org, na sisi tutakuongeza nembo yako kwenye tovuti yako haraka iwezekanavyo.

Kubadili Kichwa cha Tovuti yako

Hivyo nembo yako itaonekana juu ya tovuti ya asasi yako, na jina, mji, na ina links zinazoshirikisha tovuti yako inonekane na watu wengi zaidi kwa njia ya barua pepe, Facebook, au Twitter.

Kwenye Kichwa cha toviti utapata sehemu ya kubadili kile kinachoonekana katika kichwa.

Ukipenda unaweza kuchukua kichwa na picha yako mwenyewe kwa kubonyeza Custom header image na kuchagua picha kutoka kwa kompyuta yako.

Kubadili Muonekano wa Tovuti yako

Kubadili muonekano au rangi ya tovuti ya asasi yako kwenye Envaya, nenda chini ya sehemu Website Theme.

Chagua mandhari au muonekano unayoipenda, kisha bonyeza kitufe cha bluu ili kuhifadhi mabadiliko ya tovuti yako.