Hawa ni baadhi ya watoto waliojengewa uwezo wa sanaa na kundi la Dira.
Baadhi ya timu ya Dira wakiwa katika picha ya pamoja. hii ni katika ziara ya kutoa elimu kwa njia ya sanaa vijijini.
Wananchi katika kijiji cha Kitange Moja, wakifuatilia kwa makini moja ya kazi za sanaa zilizokuwa zikioneshwa na Dira Theatre.
WanaDira wakitoa elimu kwa jamii kwa njia ya Igizo, hii ni katika kijiji cha Mtumbatu.
Wasanii wa Dira Theatre Group wakitoa elimu kwa njia ya sanaa ya ngoma, katika kijiji cha Magubike.
Timu ya Dira Theatre Group na wasamaria wema wakisaidiana kuinasua gari walilokuwa wakisafiria lililokwama kwenye tope. Hii ni katika kijiji cha Ibindo, wilayani Kilosa.
Timu ya Dira Theatre Group katika harakati za kuifikia jamii vijijini. Hapa wakilazimika kutembea kwa miguu baada ya gari lao kukwama kutokana na ubovu wa barabara. Hii ni kuelekea kijiji cha Inyunywe, wilaya ya Kilosa.
Viongozi wa Dira Theatre Group, kutoka kushoto, Asha waziri, Erasmo Tullo, Deogratius swai na Saada Juma, katika pilika za uelimishaji wa jamii vijijini.
Viongozi wa Dira Theatre na washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja, kata ya Rudewa, wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Dira Theatre na washiriki wa mafunzo ya sera na sheria za ardhi kutoka vijiji vya kata ya Kimamba,wilayani Kilosa mkoani Morogoro.